January 13, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NELICO yaomba wadau kuungana kupinga ukatili wa kijinsia Geita

Na Mutta Robert, TimesMajira Online, Geita

Shirika lisilo la kiserikali la New Light Children Centre Organization (NELICO) limesema linalaani vikali vitendo vya ukatili ambavyo vimekuwa vikiripotiwa katika jamii ndani ya Mkoa wa Geita na kuwataka makundi yote katika jamii kushirikiana kupinga na kutokomeza ukatili miongoni mwao.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa NELICO Paulina Alex leo Juni 29,2022 wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya kikakati ya kupinga ukatili wa kijinsia yaliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Alphendo Mjini Geita.

Mafunzo hayo yamejuisha makundi mbalimbali yakiwemo madiwani,Waendesha mashitaka,Polisi,Dawati la jinsia,Maafisa ustawi wa jamii,Mahakimu ,Mawakili wa kujitegemea pamoja waandishi wa habari.

Akizunguza katika mafunzo hayo, Paulina Alex amesema kuwa matukio ya ukatili kama vile ubakaji,ulawiti ,mauaji,vipigo au aina nyingine vimekuwa vikiripotiwa sana katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Geita hivyo ameitaka jamii kujitokeza hadharani na kupinga ukatili ili isiwe sehemu ya Mila na desturi ya jamii .