January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Neema yaishukia Chuo Cha Maji

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu ametoa kiasi cha Sh 1.5 bilioni Kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu mbalimbali ikiwemo mabweni matano ya kulala wanafunzi ya Chuo cha Maji.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Maji,Jumaa Aweso alipofanya ziara ya kutembelea miundombinu ya chuo hicho na kuongea na menejimenti pamoja na wanafunzi alisema wamepewa fedha hizo ambazo zitasaidia kuboresha miundombinu hiyo ya chuo.

Waziri Aweso amesema baada ya Mhe Rais kusikia changamoto ya uchakavu wa miundombinu ya majengo hivyo aliguswa na kutoa kiasi cha Sh 1.5 bilioni kwa ajili ya kutatua kero hiyo.

“Nimeanza na Blok F kukarabati na mmeona tumefanikiwa na nina salamu zenu ambapo nimefanya mazungumzo na Mhe Rais Samia Hassan Suluhu na akaniuliza majengo yapo mangapi na nikamjibu yapo matano ndipo akanipatia kiasi cha Sh 1.5 bioni hivyo mzigo wenu unaingia Februari 28 yaani jumatatu ijayo mwaka huu,”amesema Aweso

Aidha, Waziri Aweso amekitaka Chuo cha Maji kuingia kwenye ushindani hivyo kufanya tafiti za maji na zisihishie kwenye makabati Kwa kuwa sekta ya maji ina kazi kubwa.

Katika hatua nyingine Mheshimiwa Aweso ameweka bayana kuwa amedhamiria kukipa kipaumbele Chuo hiki ambacho lengo lake ni kuzalisha wataalamu bora hivyo kukifanya kiwe miongoni mwa vyuo vitatu bora vinavyotajwa nchini.

Awali Mkuu wa Chuo hicho,Dr Adamu Karia amesema wana mapendekezo matatu ikiwemo ukarabati wa majengo ya chuo ambayo ni chakavu na yamejengwa katika miaka ya 1970 na 1980, kuongezewa bajeti ya chuo na pamoja na kupatiwa kituo cha tafiti cha Ngurdoto

Aidha Dk Kariaamemuomba Waziri kuidhinisha Kituo cha Utafiti cha Ngurdoto kilichopo Mkoani Arusha kiwe chini ya Chuo hicho ili kitumike katika Tafiti zao na Waziri ameridhia na sasa anakwenda kuwakabidhi rasmi Jumapili hii tarehe 27/02/2022 mkoani Arusha.