May 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NEEC yataja utekelezaji vipaumbele tisa mwaka wa fedha 2023/24

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

KATIBU MTENDAJI wa Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) Beng’i Issa ametaja vipaumbele tisa vitakavyotekelezwa na Baraza hilo kwa mwaka 2023/24.

Akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji na mikakati ya taasisi hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2023/24 Issa ametaja vipaumbele hivyo  kuwa ni pamoja na kukarabati vituo vya Uwezeshaji katika Halmashauri ambazo ni  Halmashauri ya Nyang’wale, Mlele na Mbinga.

Ametaja vipaumbele vingine kuwa hi  kuingia makubaliano na Chama cha Wakandarasi Tanzania ili kuboresha shughuli za ujenzi kwa walengwa wa miradi ya ujenzi hapa nchini,kuingia makub na shirika la misaada la Marekani USAID katika kuboresha maeneo mbalimbali ya wafanyabiashara hapa nchini na 

uendeleza makubaliano na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ili kuwajengea uwezo wananchi katika masuala ya usimamizi wa fedha ili kuleta tija katika masuala ya kiuchumi.

“Pia  Baraza litaboresha mfumo wa uratibu kidigitali wa ukusanyaji na uchakataji taarifa ili kutoa ripoti ya kitaifa, litatekeleza programu ya kuongeza ushiriki wa wanawake na vijana katika manunuzi ya umma kwa kuendesha mafunzo maalum jinsi ya kutumia mifumo mbalimbali ya manunuzi na pia Baraza litaendeleza na kumaliza urasimishaji wa biashara za wanawake na vijana nchi nzima, hii itasaidia wafanyabiashara kupata mikopo na mafunzo ya biashara.”amesema na kuongeza kuwa 

“Vile vile vipaumbele vingine ni  kuunganisha mifuko ya uwezeshaji katika utoaji wa mikopo na dhamana katika taasisi za kifedha zinazotoa mikopo na kuendeleza  vikundi vyote vya kifedha nchini kama vile VICOBA katika kuvishauri na kuvihamasisha na kutatua changamoto zao ili vikue.”

Akielezea mafanikio ya Baraza hilo amesema,hadi Machi, 2023  mikopo yenye thamani ya Shilingi trioni 6.1 ilitolewa kwa wajasiriamali 8.6milioni  ikiwa wanawake ni 4.7 na wanaume 3.9

Aidha amesema,Baraza linaratibu jumla ya Mifuko 72 inayotoa mikopo ya moja kwa moja, dhamana, ruzuku na programu za uwezeshaji ambazo zilitengeneza jumla ya ajira 17.6 milioni  ambapo ajira kwa wanawake zilikuwa 9.2 (52.5%) na ajira kwa wanaume ni 8.3 (47.5%).

Kwa mujibu wa Issa,hadi kufikia mwezi Juni 2023, jumla ya ajira 145,245 zimezalishwa kwa Watanzania kupitia miradi mbalimbali ya uwekezaji ambapo wanawake  ni 29,049 (20%) na wanaume 116,196 (80%) jumla 

ya makampuni ya Kitanzania 2, 010 yamenufaika kwa kupata kazi mbalimbali katika miradi inayosimamiwa na kuratibiwa na Baraza.

Aidha amesema,mafanikio katika kuendeleza viwanda vidogo na kati lengo kubwa ni kutoa fursa kwa Watanzania  kuanzisha na kuendeleza viwanda vidogo na vya kati, kupata mikopo yenye riba nafuu hususan kwa viwanda vinavyochakata mazao ya kilimo na mifugo.

” Hadi Juni 2023  mikopo yenye thamani ya Shilingi bilioni 3.8 ilitolewa kwa miradi 65 katika mikoa 13.”amesema Issa

Pia amesema BBara hilo limefanikiwa kwenye uendelezaji wa Vituo vya Uwezeshaji huku akisema nia ya Serikali ni kuhakikisha huduma za kuwawezesha wananchi kiuchumi zinapatikana karibu na wananchi pia kupatikana katika sehemu moja inayotoa  mikopo, mafunzo, urasimishaji wa biashara, ujuzi kwa wafanyabiashara, uongezaji thamani ya mazao, elimu ya kodi na upatikanaji wa masoko.

Issa amesema hadi Machi, 2023 jumla ya vituo vya uwezeshaji 18 vimeanzishwa katika mikoa 6 ya Shinyanga , Geita, Singida, Rukwa (Sumbawanga), Kigoma na Dodoma ambapo vituo viwili Morogoro na Pwani viko kwenye hatua za kuongeza huduma wezeshi na kuweza kuwa vituo vya uwezeshaji kamili.