Na Judith Ferdinand, Timesmajira Online
Watumishi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara wametakiwa kuzingatia miiko na utunzaji siri za Serikali pamoja na kuongeza ari ya utendaji kazi na utekelezaji wa majukumu ya Bodi hiyo ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi.
Akizungumza katika kikao cha Wajumbe wa Menejimenti na Watumishi wa Bodi ambacho kimefanyika mkoani Singida, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Ludovick Nduhiye, amesema utoaji siri za Serikali ni jambo la hatari ambalo linaweza kuleta madhara na taharuki kwa jamii.
Akizungumzia kikao hicho ameeleza kuwa kitasaidia kubadilishana uzoefu, kujenga mshikamano na kuchochea morali ya ufanyaji kazi kwa watumishi hivyo kuongeza tija na ufanisi katika utendaji kazi wa bodi hiyo.
Hata hivyo dhi ya viongozi na watumishi ambao wamehudhuria kikao hicho wameeleza umuhimu wa utunzaji siri na madhara ya kutofanya hivyo.
Sanjari na hayo wamewapongeza viongozi wa bodi hiyo kwa kuona haja ya kuwa na kikao kicho ambacho wanaamini kitakuwa mwarobaini wa kuondoa dosari zinazoweza kujitokeza katika utendaji kazi wa kila siku.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba