November 8, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ndele Mwaselela amsemea mazuri  Rais Samia kwa wanawake wajasiliamali

Na Esther Macha,Timesmajira,online, Mbeya

MKURUGENZI wa shule ya Paradise Mission Pre&Primary School ,Ndele Mwaselela  amesema kitendo cha wanawake wa Mkoa wa mbeya kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika mambo ya uchumi  kwa namna hiyo wameonyesha wazi kuwa kumuunga mkono kwa vitendo hasa masuala ya uchumi

Amesema kuwa wanawake wa mkoa wa Mbeya kupitia wanawake wote nchini wamefanya jambo la msingi kwa kufanya mambo yao  kwa vitendo katika masuala ya kujiongeza kiuchumi.

Mwaselela amesema hay leo wakati akizungumza na wanawake wajasiliamali kutoka kata mbali mbali zilizopo mkoani hapa ikiwa ni sehemu ya kuwapa elimu ya ujasiliamali kupitia wataalam mbali mbali kutoka taasisi za fedha .

“Mimi wiki nzima nilikuwa bize na ubize wenyewe ulikuwa nikuongea na wanawake tu ukienda huku wanawake wanafungua vikundi ,mara elimu ya ujasiliamali kwa namna hiyo mmeonyesha nia na uthubutu kumuunga mkono kiuchumi Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan , niwaombe wanawake kuendelea kuombea nchi yetu kwasababu mwanamke mwezenu Rais Samia ameonyesha  uthubutu  wa hali ya juu na mfano mkubwa katika kupambania maendeleo  ya  watanzania na walio wengi ni wanawake hilo pekee linawapa nguvu nyinyi wanawake kuendelea kumsemea vizuri kila wakati na kila saa kuhakikisha Rais Samia anaendelea kutimiza ndoto zake kwa watanzania hasa kupitia kundi kubwa la wanawake “amesema Mwaselela.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo alisema Rais Samia amekuwa  akisisitiza umoja na mshikamano  ,upendo na utulivu wa nchi hivyo  na kuwaomba wanawake kuwa sehemu ya kushikamana na kupendana  ili kuweza kutimiza agano lao la kukuza uchumi wa mwanamke bila kujali itikadi za vyama vyao na dini zao.

“Ndugu zangu nyie wanawake  nyie ni kundi kubwa sana  naomba muendelee kumuunga mkono kwa kutangaza mambo makubwa aliyofanya na hasa kwenye mikoa yote ya Tanzania mmeona Rais akijipambanua  katika maendeleo ya mtu mmoja mmoja na maendeleo ya vikundi na jamii isiweze kutumbukia katika majanga mbalimbali ,amekuwa mtu mwema katika hali ya kawaida kila mara anawaza huduma ambazo zinalenga wananchi na kuwapunguzia mizigo  na adha kwa wananchi ,mwaka huu ametoa fedha ambazo zimegusa kila mkoa  na kila aina sekta”amesema Mkurugenzi huyo.

Akielezea zaidi Mwaselela amesema kwamba  kuna uboreshaji wa miundo mbinu pia unaenda kwa kasi mkoani hapa na kwamba kuboreshwa kwa miundo mbinu kutasaidia kasi kubwa ya kukua kwa uchumi .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi cha wajane kilichopo kata ya uyole ,Suzana Mchiwa amesema  kwamba waliamua kuanzisha kikundi hicho cha ujasiliamali baada ya kujikuta wanamaisha magumu ambayo yalipelekea baadhi yao kushindwa kumudu maisha na wengine kushindwa kusomesha watoto baada ya wao zao kufariki.

“Hiki kikundi tunajishughulisha na kazi  mbali mbali mfano kuuza maharage ,kulima viazi ,kusuka mikeka na shughuli zingine za kujiongezea kipato hivyo tunamuomba ndugu mgeni rasmi Ndele Mwaselela atusaidie kupata mitaji ambayo itaweza kutuinua zaidi ya hapa”amesema Mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake Mwanasheria wa kujitegemea  wa Kampuni ya Aika  Attorners ,Aikande  Lema amesema kuwa aliwataka wanawake kuacha woga  na kusema kuwa uvumilivu upo lakini si kila jambo  na kwamba lengo  ni kujitengeneza na jamii9 inayojitambua.