Na Agnes Alcardo,TimesmajiraOnline, Simiyu
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Balozi Emmanuel Nchimbi,anatarajiwa kuanza ziara yake ya siku saba katika Mikoa miwili ya Simiyu na Shinyanga.
Katika ziara hiyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020/2025,kuangalia uhai wa CCM, mwenendo kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kutatua na kusikiliza kero za wananchi.
Dkt.Nchimbi kesho Oktoba 6, 2024 ataongozana na Katibu wa NEC, Itikadi, Uendezi na Mafunzo CCM Taifa, CPA Amos Makalla pamoja na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Rabia Abdallah Hamid.
Kwa mujibu wa taarifa inaeleza kuwa, ziara hiyo itaanza kesho Oktoba 6, Mkoani Simiyu hadi Oktoba 11, 2024 kumalizia Mkoani Shinyanga.
Aidha lengo lingine la ziara hiyo limeelezwa kuwa ni kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la mkazi na kujiandikisha kupiga kura.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria