December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Nchimbi awasili Mtwara,awasisitiza wanaccm kushikamana

Na Penina Malundo, Timesmajira

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, leo amewasili Mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi ya siku tano huku akiwataka wanachama wa CCM kuwa madhubuti kushikamana, kupendana,kushirikiana na kutambua kuwa wanawajibu wa kuwatumikia watanzania kwa nguvu zote.

Hayo ameyasema leo baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Masasi,amesema wao wanaamini umoja na utulivu unategemewa sana na Chama hicho katika kuwa madhubuti.

Amesema wanaccm wanawajibu wa kupata viongozi wazuri ambao wanamoyo wa kuwatumikia wananchi..”wale wazuri miongoni mwetu wapewe nafasi ya kuongoza kwenye jamii.

“Wanaccm wanajukumu la pekee la kuchujana kuhakikisha wanapata viongozi wazuri ambao wanapata nafasi ya kuongoza jamii ambao tunategemea tukiwapa heshima hiyo wataleta heshima ya CCM na nchi yetu ,”amesema

Dkt.Nchimbi amefurahishwa na umoja waliouonyesha wanaccm wa Masasi kwa namna walivyojitokeza kwa wingi katika mapokezi.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa-NEC, Oganaizesheni, Issa Usi Haji Gavu, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA- Amos Makalla na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa-SUKI- Rabia Hamid Abdalla.