*Aleleza mipango ya CCM kwa Wilayanya Sumbawanga endapo kitashinda
Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online-Sumbawanga
MGOMBEA Mwenza wa kiti cha Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ameendelea ‘kuchanja mbugu’ katika maeneo mbalimbali nchini, akizisaka kura za CCM ili kiweze kushinda katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.
Akiwahutubia wananchi wa Sumbawanga mjini, mkoani Rukwa,Dkt.Nchimbi amewaelezea mipango mikakati iliyokusudiwa kufanywa na chama hicho, endapo kitaingia tena madarakani ikiwemo uboreshwaji katika sekta ya afya, elimu, kilimo na miundombinu ya barabara.

Amesema, katika Wilaya ya Sumbawanga Mjini, kwenye upande wa afya, CCM imedhamiria kuongeza vituo vipya vya afya vitatu,zahanati nane na magari ya wagonjwa matano ili kuendelea kupunguza changamoto wanazokumbana nazo wananchi kwa upande wa afya.
Akizungumzia upande wa elimu, Balozi Nchimbi amesema, Serikali chini ya CCM imedhamiria kujenga shule za sekondari mbili na msingi nane zitakazokuwa na madarasa 188 katika wilaya hiyo.
Aidha amesema, katika upande wa kilimo, upo mpango wa kuongeza skimu za umwagiliaji tatu, kuongeza uchimbaji wa mabwawa 220 na vizimba vya kufugia samaki 30,kuongezwa kwa kongani ya viwanda katika Mkoa wote wa Rukwa, hali itakayoleta tija katika maendeleo ya nchini.
Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, hapo baadae anatarajiwa kuwahutubia wananchi wa Maji Moto mkoani Katavi, ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni za CCM zinazoendelea nchini.


More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako