March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NCCR Mageuzi kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani

Na Mwandishi wetu ,Timesmajira

CHAMA cha NCCR Mageuzi kimesema kuwa kipo tayari kushiriki uchaguzi hakitatamani kuona taharuki ama kuvurugika kwa amani ndani ya nchi na Taifa kwa ujumla.

Kinapinga maandamano ya aina yeyote ile isipokuwa maandamano yao mtayaona kwenye masanduku ya kura ambapo watajitokeza kwa wingi Ili kupiga kura zakuleta mabadiliko na Mageuzi.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam Katibu mkuu wa chama hicho Evaline Munisi amesema wameamua kwa ridhaa yao kushiriki kinyanganyiro cha kuleta ukombozi nchini Tanzania.

” Kwa kudhibitisha hilo hadi hivi sasa hatunapingamizi lolote  kuhusu uchaguzi hivyo chama chetu kina imani haki inaatendeka ambapo kila atayeshinda atatangazwa kwa mujibu wa Sheria ya Tume huru ya Taifa ya uchaguzi,” amesema Munisi.

Aidha Munisi amesema kwa hayo yote ni matunda na matokeo ya mlezi uwa vyama vya siasa ndugu jaji Francis Mutungi kongole sana kwake ambapo ushirikishwaji kwa masuala yanayohusu uendeshaji wa vyama vya siasa .

Mkuu huyo ameeleza kuwa toka kampeni za uchaguzi kuanzia hawajasikia matatizo yeyote juu ya uendeshaji wa kampeni hizo hivyo amani na mshikamano uliokuwepo kwa watanzania 

Hata hivyo Kuna baadhi ya watu wanafanya chokochoko na kusababisha taharuki kwa watanzania wanahamasisha kutotii Sheria na kupandikiza chuki kwa watanzania Ili kuyumbisha msimamo wa Dola.