December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NBC yapongezwa kwa huduma bora Zanzibar

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdullah ameipongeza Benki ya NBC kwa kuendelea kutoa huduma bora za kifedha kwa wananchi wa Zanzibar na taifa kwa ujumla.

Mheshimiwa Abdulla aliyasema hayo wakati Akizungumza na viongozi wa Benki ya NBC alipokutana nao katika ofisi ya Spika mjini Unguja, mara baada ya viongozi hao kuhudhuria kikao cha baraza la Wawakilishi wakiwa ni wageni wa Spika wa Zanzibar, Mheshimiwa Ally Zubeir.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi akizungumza wakati wa Mkutano wake wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulah na Spika wa Zanzibar Ally Zubeir walipokutana Zanzibar hivi karibuni.

“Nawapongeza sana NBC kwa kuendelea kuwa mdau muhimu wa uwezeshaji wa kiuchumi kwa watu wa Zanzibar. Endeleeni kuongeza wigo wenu wa kutolea huduma kwa kuongeza matawi na Mawakala ili muweze kuwafikia wananchi wengi zaidi. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawaahidi ushirikiano na kuendelea kuweka mazingira bora ya kufanyia biashara” alisema.

Kwa upande wake Spika wa Zanzibar, Mheshimiwa Ally Zubeiry, aliishukuru Benki ya NBC kwa kuendelea kuwa mdau mkubwa wa maendeleo akitolea mfano misaada mbalimbali kwa jamii ambayo Benki hiyo imekuwa ikitoa kila mwaka.

Spika Zubeiry alisifia pia udhamini wa Benki ya NBC katika ligi ya mpira wa miguu nchini, NBC Premier league kuwa ni wenye tija kwa taifa kwa kutoa vipato na kuibua vipaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi alimshukuru Makamu wa Pili wa Rais Mheshimiwa Abdulla na Spika wa Zanzibar Mheshimiwa ZUbeiry kwa mkutano huo wenye lengo la kuboresha mahusiano ya pande zeto..