January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NBC yaendelea kukuza ushirikiano kupitia ibada ya iftari

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Theobald Sabi amesema NBC inaendelea kukuza mshikamano na maelewano katika familia na jumuiya kupitia ibada ya iftari.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya Iftar kwa wateja wa NBC wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sabi amesema benki ya NBC imeamua kufanya tukio hili kwa ajili ya kukuza mshikamano na maelewano katika familia na jumuiya.

Sabi amesema, “tunaamini kufunga ni mafunzo, yanaleta maisha ya ukarimu, uchamungu, ukweli, furaha na mshikamano baina ya jamii,”

“Tunawashukuru wateja wetu kwa kuitikia wito na kuwa pamoja nasi katika hafla hii muhimu ya Iftar kwa ajili ya kurudisha kwa mwenyezi mungu kupitia ibada ya upendo, kutoa zaka na sadaka,”amesema

Aidha, Sabi ameendelea kuhamasisha watu binafsi na taasisi kuendelea kuwasaidia watu wengine kupitia ibada mbalimbali.