October 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka

Nanenane kitaifa kufanyika Simiyu

Judith Ferdinand, Mwanza

MAONESHO ya Sikukuu ya wakulima (Nanenane) kitaifa yamepangwa kufanyika Mkoani Simiyu huku wadau pamoja na taasisi mbalimbali zikiwemo wa sekta ya Mifugo na Uvuvi kutakiwa kujitokeza kwa wingi.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka wakati akizungumza kwenye kikao cha kutoa taarifa ya maendeleo ya mifugo na uvuvi ya Mkoa huo kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega ambaye yupo Mkoani humo kwa ziara ya siku mbili .

Mtaka amesema, Nanenane ipo baada ya Wizara na taasisi zote za kiserikali kukubali kushiriki hivyo wajasirimali wakubwa na wadogo watumie fursa hiyo kupeleka bidhaa zao pamoja na Wizara hiyo ya Mifugo na Uvuvi kushiriki kama ilivyoshiriki mwaka jana na kuwa vivutio.

“Napenda kutumia fursa hii kwa taarifa zinazotolewa kwenye mitandao ya kuwa maonesho ya nanenane mwaka huu hayatafanyika kutokana na corona kuwa ni batili hivyo nautaarifu umma kuwa, maonesho haya kitaifa yatafanyika Mkoani hapa na yatafunguliwa na kufungwa na viongozi wa kitaifa na tayari taasisi mbalimbali za kiserikali zimethibitisha kushiriki,” amesema Mtaka.