April 1, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Nane mbaroni tuhuma za kukutwa na dola bandia

Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza

Watu 8 wamekatwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa tuhuma za kukutwa na noti bandia 9740 za dola 100, walizotaka kuziingiza kwenye mzunguko halali wa kifedha.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mwanza Machi 28,2025,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa,amesema Machi 1,2025,majira ya saa 7:30 mchana, eneo la Kemendo Kata na
Wilaya ya Nyamagana, mkoani Mwanza,walipata taarifa juu ya kuonekana kwa watu wakiwa na
kiasi kikubwa cha fedha bandia za kigeni.

Mutafungwa amesema,baada ya kupata taarifa hizo waliandaa mpango kazi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa na notice hizo bandia akiwemo Frank Joseph(34), Mkazi wa Mtukula mkoani Kagera,Augustino Mambo(32),mfanyabiashara na mkazi wa Dodoma na Lau Wanjara (45) fundi na mkazi wa Wilaya ya Ilemela mkoa wa Mwanza.

Wengine ni Isaya Ndilihungwa(61), mganga wa tiba asilia na mkazi wa Dar-es-Salaam, Cleophas Magoti(40) mkulima na mkazi wa Makondeko, mkoa wa Morogoro,Jeronimo, Method Injinia(34) mfanyabiashara na mkazi wa Mkolani jijini Mwanza.

Pamoja na Joseph Rhobynson(42) mfanyabiashara na mkazi wa Nyamh’ongolo,
wilayani Ilemela na Wilberd Frances(32) mkazi wa Dar-es salaam.

“Tunaendelea na uchunguzi kwa kushirikiana na taasisi nyingine, ili kuweza kubaini mtandao wa wahalifu hao, hata hivyo watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka matatu ambayo ni kutakatisha fedha, kupatikana na fedha bandia na uhalifu wa kupanga katika kesi ya uchumi namba 7118/2025,”.