December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Nandy

Nandy athibitisha kutolewa barua

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri hapa nchini kwa upande wa wanawake Faustina Charles maarufu ‘Nandy’, amethibitisha kutolewa barua na aliyekuwa mpenzi wake Billnass.

Akithibitisha hilo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram Nandy amesema, kwa sasa yeye ni mke mtarajiwa kwani tayari ameshatumiwa ujumbe kuwa barua ya mpenzi wake aliyepeleka kwao imepokelewa.

“Nimepokea ujumbe kuwa barua yake imepokelewa nyumbani. Hivyo kwa sasa mimi ni mke mtarajiwa (wife to be),” ameandika Nandy kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram.