Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Dkt.Festo Dugange amesema kuwa Vyuo vingi nchini vinakabiliwa na Changamoto ya matokeo ya tafiti nyingi kuishia kwenye machapisho ya kitaaluma na kubakia kwenye makabati ofisini na hazifikishwi kwa walengwa.
Dkt.Dugange amesema hayo jijini hapa leo,Disemba 5,2024 wakati akimuwakilisha Waziri wa TAMISEMI,Mohamed Mchengerwa kwenye Mahafali ya 16 ya Chuo cha Serikali za Mitaa(LGTI)-Hombolo yaliyofanyika katika Kampus kuu ya chuo hicho.
Ambapo amesema ili tafiti ziweze kuwa na manufaa lengwa ni lazima matokeo na mapendekezo ya tafiti hizo yawafikie walengwa hivyo ni utoaji wa matokeo ya tafiti yakatolewe kule tafiti zilipofanyika ili walengwa, wananchi, viongozi na watendaji watakaohusika na matumizi ya matokeo ya tafiti hizo wawepo.
“Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini bado zinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na uhaba wa wataalamu, ukusanyaji mdogo wa mapato na usimamizi usioridhisha wa utekelezaji wa miradi ya kimkakati kwa baadhi ya Halmashauri, pamoja na shughuli nyinginezo.
“Chuo cha Serikali za Mitaa kina nafasi na jukumu kubwa la kuisaidia Serikali katika kutatua changamoto hizo kupitia mafunzo, tafiti na ushauri wa kitaalamu,”amesema Dkt.Dugange.
Ameeleza kuwa bado mafunzo, tafiti na ushauri elekezi vina nafasi kubwa kusaidia katika kubaini namna ambavyo changamoto za Mamlaka za Serikali za Mitaa zitakavyoweza kutatuliwa kwa kutoa wataalamu waliopikika vizuri, kufanya tafiti zinazolenga kutoa majibu katika changamoto hizo, lakini pia kutoa mafunzo ya muda mfupi yenye kuleta mabadiliko chanya katika utendaji.
“Napongeza jitihada za Chuo hiki kuendelea kufadhili tafiti kila mwaka zinazolenga kutatua changamoto mbalimbali katika Serikali za Mitaa lakini matokeo ya tafiti hizo yakatolewe kule kwa wananchi ambao walihisika kufanyiwa tafiti ili wafahamu changamoto ya maeneo yao na kuona namna wanavyoweza kuzitatua” amesema Dkt. Dugange.
Dkt.Dugange mapema leo ameunda mahafali ya 16 ya Chuo cha Serikali za Mitaa yaliyofanyika kwenye Kampasi kuu ya Chuo hicho ambapo katika Mahafali hayo wanafunzi 4,650 wamehitimu kozi mbalimbali kwa ngazi ya Astashahada ya awali, Astashahada ya Kati pamoja na Shahada katika fani mbalimbali.
More Stories
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam
MSF ilivyojidhatiti kusaidia serikali katika utoaji wa huduma za afya
Prof.Muhongo awapongeza vijana 32 waliotembea kwa miguu kutoka Butiama hadi Mwanza