December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Naibu Waziri na Mbunge wa kuteuliwa ajiuzulu ubunge



Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline

MBUNGE wa kuteuliwa na Rais na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, amejiuzulu ubunge.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge, ilieleza kwamba Balozi Mbarouk, amemuandikia Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson barua ya kujiuzulu Ubunge jana,  Julai  21 , 2024.

Kwa mujibu ya barua aliyomuandikia Spika, Balozi Mbarouk alisema amefikia
uamuzi huo kufuatia changamoto za kijamii zinazomkabili kwa sasa.

“Ninalazimika kuchukua uamuzi wa kujiuzulu ili nipate nafasi ya kushughulikia
changamoto hizo,” alisema Balozi Mbarouk katika barua yake ya kujiuzulu Ubunge.

Kea Uamuzi huo, Mbarouk anapoteza sifa ya Kuwa naibu   waziri, huku Uamuzi huo ukimpa Rais Samia Suluhu Hassan ya kuteua MBUNGE mwingine wa kuteuliwa na Rais.

Kwa mujibu wa Katiba yabJamhuri ya Muungano anayo nafasi ya kuteua wabunge 10.
21 Julai, 2024.