November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Naibu waziri Mary awataka Wanawake kuchagamkia fursa katika sekta ya utalii.

Na Mwandishi wetu Timesmajira online

KATIKA Kuelekea siku ya maadhimisho ya wanawake duniani ambayo uadhimishwa Kila ifikapo Machi 8 wanawake wameaswa kutumia fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja kuwekeza katika sekta ya utalii ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Wito huo umetolewa Jijini Dar es salaam jana na Naibu Waziri wa Maliasiri na utalii Mary Masanja katika hafla iliyowakutanisha wanawake, wafanyakazi na watendaji wa Kijiji cha makumbusho.

“Wanawake wamekuwa wakishiriki katika ujenzi wa masuala mbalimbali hivyo nawaomba pia kuwekeza katika sekta ya utalii kwani inafursa nyinyi ambazo zitawawezesha kupata kipato” amesema Masanja.

Masanja amesema kuwa wanawake wamekuwa wakishiriki katika maeneo mbalimbali hivyo watumie fursa ya utalii kwa kutenegeza vitu vya asili ambavyo vitawasaidia kujipatia kipato.

Kwa upande wake Muhifadhi katika Kijiji cha Makumbusho,Agnes Robati amesema kijiji cha Makumbusho kimekuwa kikitoa elimu kwa wananchi kuhusu kutambua urithi wao ikiwa ni pamoja na kutumia vyakula vya asili,kujua mila na desturi na ngoma za asili.

‘Lengo letu ni kuhakikisha kwamba jamii nzima wakiwemo watoto wetu wanatambua umuhimu wa utalii, ikiwemo fursa mbalimbali ambazo zinapatikana na hatimaye kujiongezea kipato”amesema

Arietha Bernad ni mmoja wa washiriki katika hafla hiyo amesema katika kudumuisha siku ya wanawake amekuwa akitumia juhudi kufanya shughuli za ujenzi ambazo amerithishwa na wazazi wake .

Aidha aliwataka awanawake kutolemaa badala yake washiri katika ujenzi kwani ni miongoni mwa fursa inayoweza kumuingizia kipato na kunyanyua uchumi wake.

Pia aliwataka watanzania kutumia utamaduni wa kutumia na kula vyakula vya asili ili kuendeleza mila na desturi kwa jamii na hivyo kufanya wageni kutambua urithi wa mtanzania na sio kupenda kutumia vitu vya nje ya nchi.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja akiangalia na kukagua baadhi ya nguo ambazo zimeshonwa na wajasiriamali waliopo katika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja akiwa amevaa Kofia kichwani ambayo imeshonwa na wajasiriamli waliopo katika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam