Doreen Aloyce, TimesMajira Online, Tabora.
Naibu Waziri Wizara ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, ameiagiza Bodi ya Maghala,kuhakikisha inajenga maghala ya kisasa ili wakulima waweze kuhifadhi mazao Yao na kuongeza ubora wa mazao Yao ambayo yatapata Bei nzuri.
Akizungumza Leo alhamisi katika uzinduzi wa siku ya stakabadhi za ghala katika Maadhimisho ya siku ya Ushirika Duniani yanayofanyika Kitaifa mkoani Tabora,amesema kuwa Kuna umuhimu mkubwa wa wakulima kuyahifadhi mazao Yao sehemu salama ambayo yatakuwa na ubora na Bei nzuri.
Amesema maghala ni muhimu na ndio maana Serikali inaona umuhimu wa kiwasaidia wakulima katika kuhifadhi mazao Yao kutokana na changamoto ya baadhi Yao kushindwa kuhifadhi mazao Mahali pa uhakika.
Amebainisha kuwa kwa kutaka kuwasaidia wakulima ndio maana Serikali inasisitiza umuhimu wa mfumo wa stakabadhi ghalani ambao una manufaa makubwa kama mkulima kuuza mazao yake kwa Bei ya soko,kuhifadhi mazao sehemu salama na uhakika wa takwimu.
“Dunia kwa Sasa Ina ushindani wa soko ,hivyo ni muhimu kuwa na mfumo unaoeleweka kama wa stakabadhi ghalani ambao pia unatoa uhakika wa chakula”Amesema
Ametoa mfano wa ongezeko la Bei ya mazao tangu kuanzishwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani kuwa ni asilimia 257 kwa zao la Choroko,asilimia 250 kwa zao la Kakao na asilimia 168 kwa zao la korosho.
Kwa upande wa changamoto,ameeleza kuwa bado Kuna uelewa finyu kuhusu manufaa ya stakabadhi ghalani na uhaba wa maghala na ndio maana wameagiza ujenzi wa maghala kuwasaidia wakulima na elimu kuendelea kutolewa kwa wananchi na wakulima kuhusu manufaa ya mfumo huo.
Mrajis wa Vyama vya Ushirika Nchini,Dk Benson Ndiege,amewasisitiza wakulima kuchangamkia mfumo wa stakabadhi ghalani ambao Bei inakuwa nzuri kwa vile mazao yanakuwa Bora.
Amewataka watumishi katika sekta ya Ushirika kutofanya kazi kwa njia ya ujanja ujanja Bali kwa uaminifu ili Ushirika iwe na manufaa kwa wanaushirika.
Hata hivyo uzinduzi huo ulienda sambamba na ugawaji wa zawadi kwa vinara waliofanya vizuri hususani utunzaji wa maghala
More Stories
Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini yafanya ziara ya kujifunza uongezaji thamani wa madini nchini Zambia
Rehema Simfukwe atoboa siri sababu kuimba wimbo wa Chanzo
Tanzania ipo tayari kupokea wakuu wa nchi,mkutano wa nishati-Dkt.Kazungu