Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Pauline Gekul amekutana na viongozi wa wanawake katika michezo na kujadiliana mambo mbalimbali kuhusu kuendeleza michezo nchini.
Akizungumza na viongozi hao leo Februari 23, 2022 kwenye Ukumbi wa Uwanja wa Mkapa. Mhe, Gekul amesema viongozi hao kwa kushirikiana na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) wanapaswa kufufua michezo isiyofanya vizuri ili iwe kama awali.
Amelielekeza BMT kusimamia uchaguzi wa viongozi wa CHANETA kuanzia ngazi ya chini hadi taifa ili usimamizi wa michezo nchini uweze kuimarika.
“Ndugu zangu lazima tuambiane ukweli bila uongozi imara hakuna michezo, hivyo nakuagiza BMT hakikisha unasimamia uchaguzi ufanyike mara moja” amesisitiza Mhe. Gekul
Amelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kuwekeza zaidi kwenye timu za wanawake badala ya kung’ang’ania timu za wanaume kwa kuwa ndiyo zinazofanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya kimataifa.
Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli nchini (CHANETA) Dk, Devotha Marwa amesema mikakati iliyopo kwa sasa ni kurudisha hadhi ya mchezo huo ambapo amesema tayari CHANETA imeandaa Mpango Mkakati wa miaka minne ambao una kipaumbele kadhaa.
Ametaja baadhi ya vipaumbele ni kuwa na timu ya vijana ya Taifa, kutoa mafunzo kwa viongozi, kutafuta ufadhili, ujenzi wa ofisi pamoja na kuwa na viwanja vya michezo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu kwa wanawake nchini (TWFA) Somoe Ng’itu ameishukuru Serikali kwa kuipa kipaumbele mpira wa miguu kwa wanawake na kuahidi kukamilisha changamoto chache zinazokabili eneo hilo.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa