Na Mwandishi Wetu, Timesmajira
Kocha Mkuu wa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC, Nasreddine Nabi amesema ataingia kwenye mchezo wa kesho kwa nguvu kubwa kuhakikisha wanapata ushindi na kutinga hatua ya Robo fainali.
Yanga SC, itakuwa mwenyeji kesho katika mchezo wa mzunguuko watano wa Kundi D, Kombe la Shirikisho Barani Afrika, utakaofanyika kwenye Uwanja wa Bengamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
“Sitak kuwaangalia wapinzani wangu nini wanachotaka kukifanya katika kuelekea mchezo huo, kikosi changu kitaingia kwa nguvu zote ili kupata ushindi.
“Ninaendelea kukiimarisha kikosi changu ili kipate matokeo mazuri ya ushindi na sio kitu kingine, nimepanga kutumia wachezaji wangu wote muhimu ili kuhakikisha tunapata ushindi wa hapa nyumbani utakaotupeleka Robo Fainali,”
US Monastir tayari imefuzu Robo Fanaili ya Kombe la Shirikisho Afrika katika Kundi D ikiwa na alama 12, ikifuatia na Young Africans yenye alama 07, TP Mazembe ipo nafasi ya tatu ikiwa na alama 03 na AS Real Bamako ipo nafasi ya mwisho kwa kumiliki alama 02.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania