January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mzenji Afika Nairobi Kenya

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Rais wa Timu ya Mpira wa Kikapu ya Dar City, Mussa Mzenji amefika Nairobi Kenya na kupokelewa na mtoto wa Rais Ruto, Charline Ruto baada ya kumualika kutembelea mechi za Bonanza za mpira wa kikapu ambazo baadhi zinasimamiwa na Taasisi ya mtoto wa Rais Ruto.

Katika mualiko huo pia mgeni mwingine aliyealikwa ni Pamoja Na mtoto wa Rais wa Zimbambwe, Tariro Washe.

Hii yote ni kutokana na mafanikio ya kukuza mpira wa kikapu nchini ambayo Musa amekua akifanya kwa kipindi cha hivi karibuni baada ya kuziunga mkono Timu za kikapu za Pazi na Dar City.