November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mzee wa Yesu awaondoa hofu waumini wake

Na David John timesmajira online

ASKOFU mkuu wa Kanisa la House of Prayer Shield of Faith Christian Fellowship Mulilege Mkombo Kameka maarufu Baba Mzee wa Yesu amewaongoza waumini wa kanisa hilo kwa maombi maalum ya watu kupokea uponyaji pamoja na miujiza ya kutembea juu ya maji kwa lengo la kuwafungua vifungo ambavyo vimefungwa kimiujiza.

Pamoja na maombi hayo ya uponyaji, Baba Mzee wa Yesu ameendesha semina kuanzia Novemba 2 hadi sita ambayo imewahusisha waumini wa kanisa hilo pamoja na wananchi wa Jiji la Dar es Salaa.Semina hiyo ilikuwa ikifanyika kwenye Kanisa hilo ambalo liko Boko jijini Dar es Salaam.

Baba Mzee wa Yesu ameendesha semina na maombi hayo kwa kutumia redio Mamlaka inayomilikiwa na Kanisa hilo na sababu za kutumia redio hiyo inatokana na yeye kutokuwepo nchini Tanzania tangu Mei mwaka huu baada ya Serikali kupitia Uhamiaji kumuondoa kwa maelezo kwamba sio raia wa Tanzania.Hivyo alisema kuwa Baba Mzee wa Yesu kwa sasa anaishi nchini Congo na haifahamiki lini atarejea nchini kuungana na waumini wake.“Mungu akipenda tutaonana.”

Akizungumza na waumini na wananchi mbalimbali wakati akihitimisha semina hiyo Jijini Dar es Salaam Mzee wa Yesu kwa kutumia redio Mamlaka ya Kanisa amewaambia waumini wake iko siku Mungu akipenda wataonana ana kwa ana na kwamba mipango ya Kanisa hilo ni kuendelea kukua na kuongeza waumini wake na ifikapo mwaka 2025 watakuwa wamefikia waumini milioni mbili nchini.

Msemaji wa kanisa la house of prayer shild of Faith christian fellowship Church kuhani wa kristo Nazar Kilama akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hitimisho la semina na ujio wa Kiongozi wa kanisa hilo Mulilega Mkombo huku Hawapo pichani huku akiwa amezungukwa na makuhani wa kanisa hilo.

Pia Baba Mzee wa Yesu amewaambia waumini na wananchi kwamba Kanisa hilo ni tofauti na baadhi ya makanisa mengine ambayo yamejikita kuwatumia waumini kuchuma fedha lakini Kanisa lao limejikita kuhubiri habari ya Yesu na kutatua changamoto za wananchi kwa njia ya maombi na si kuchangishana fedha.

Kwa upande wake Msemaji wa Kanisa hilo Kuhani wa Kristo Nazar Kilama amefafanua kuwa Kanisa hilo limekuwa likiendesha semina kuanzia Novemba 2 hadi Novemba 6 mwaka huu na kabla ya kufanyika Dar es Salaam pia imefanyika mikoa ya Dodoma na Mbeya.

“Semina hii ilikuwa ni kwa ajili ya kuwezesha watu mbalimbali wa ndani ya Kanisa na nje ya Kanisa kwasababu walioshiriki semina hii sio watu wa ndani ya kanisa peke yake.Lengo la semina hii ilikuwa ni kuwaweza watu kupokea miujiza ya kutembea juu ya maji.

Nakuongeza kuwa “Kutembea juu ya maji kwa maana unatembea juu ya madui zako kwa hiyo ndio ilikuwa lengo la semina ambayo Baba Mzee wa Yesu ameifanya kwa kipindi cha Novemba 2 hadi Novemba 6.Baba Mzee wa Yesu ameendelea kutushibisha neno la Mungu kwa kupitia redio Mamlaka ambayo ni ya Kanisa.

kama mnavyojua na mnakumbuka Baba Mzee wa Yesu walimtoa hapa kipindi kile wakampeleka Congo bado hajarudi kwa hiyo alikuwa anatumia njia ya redio mamlaka kuendesha semina ambayo imefanyika kwa mafanikio makubwa.Watu wengine wamepokea ,wameona vitu ambavyo hawajawahi kuona kwenye maisha yao,”amesema.

Ameongeza kwa hiyo kuna vitu vingi ambavyo vimefanyika kwenye semina hiyo kwani watu wamefunguliwa,wameachiliwa waliokuwa wamefungwa na vifungo vua miujiza na wengine ambao kazi za mikono zilikuwa zimefungwa Baba Mzee wa Yesu amewaombea na sasa wataendelea kupokea miujiza kule wanakoelekea.

Alipoulizwa ni lini Baba Mzee wa Yesu atarejea nchini, Msemaji huyo wa Kanisa alisema kwamba Baba Mzee wa Yesu kwenye mahubiri yake ameshasema Mungu akipenda tutaonana na ya Mungu ni mengi na Mungu anaweza kufanya njia pasipo na njia.“Kwa hiyo sisi waumini, kama wasaidizi wake tumeendelea kufanya maombi ya kuomba na kumsihi Yesu afanye njia pasipokuwa na njia.Tunaamini siku moja tutakuja kumuona Baba Mzee wa Yesu, sisi ni watu wa maombi na tutaendelea kufanya hivyo kadri anavyotuelekeza.

Kwa upande mwakilishi wa Kanisa hilo kutoka mkoani Mwanza Brian Kilonzo amesema kwenye semina hiyo wamejifunza mambo mengi na moja kusikia, wamepokea sikio la Mungu.“Watu wengi wamekuwa wakipokea mambo mengi ya kidunia lakini tukija kwenye masuala ya Mungu tunakuwa wazito.

“Unafundishwa kila siku mahubiri yale yale lakini unaendelea na mambo ya kidunia kwasababu hatujapokea sikio la Mungu, kwa hiyo kwenye semina hii tumejifunza na tumepokea sikio la Mungu.Watu wanakaribishwa kwenye Kanisa la Baba Mzee wa Yesu , tunapata uponyaji wa kiroho.”