March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mzee Makamba amuombea kura Dkt.Samia, Mgombea Ubunge Bumbuli

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Tanga

KATIBU Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Yusuf Makamba,amewaomba wananchi wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga, kumchagua mgombea wa kiti cha Urais wa chama hicho,Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.

Pia, amewaomba wananchi hao kumchagua mgombea Ubunge wa Jimbo hilo kupitia CCM Mhandisi Ramadhani Singano na madiwani wote wa chama hicho, ili wananchi hao waendelee kunufaika na miradi ya maendeleo.

Makamba amesema hayo,Septemba 15, 2025 kwa njia ya simu kwenye mkutano wa kampeni za Mgombea mwenza wa kiti cha kwa tiketi ya chama hicho, Dkt. Emmanuel Nchimbi uliofanyika Lushoto eneo la Soni.Baada ya Dkt.Nchimbi kumpigia simu.

Mzee makamba amesema anaimani na wagombea wote wa CCM na alipenda kuhudhuria mkutano huo, huku akieleza kushinda kuhudhuria kwenye mkutano huo ni kutokana na changamoto ya afya yake.