Na Mwandishi Wetu, TimesMajira, Online Zanzibar
MWENYEKITI wa ZEC, Jaji Mstaafu Hamid Mahmud amemtangaza mgombea wa Urais Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dkt. Hussein Mwinyi kuwa mshindi wa Urais Zanzibar.
Matokeo hayo yametangazwa leo jioni mara baada ta majumuisho ya kura. Amesema idadi ya wapiga kura walioandikishwa kwenye daftari la kudumu ni 566,352 ambapo idadi halisi ya waliopiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu ni 498,786 ikiwa sawa na asilimia 88.07.
Mwenyekiti huyo amesema idadi ya kura halali ni 487,842 sawa na asilimia 97.81 na kura zilizokataliwa ni 10,944 sawa na asilimia 2.19.
Mwenyekiti huyo amesema Dkt.Mwinyi ameipata kura 380,402 sawa na asilimia 76.27 huku Seif Sharif Hamad akipata kura 99103 sawa na asilimia 19.87.
“Mgombea mwingine ni wa chama cha AAFP, Said Soud Said aliyepata kura285 sawa na asilimia 0.06,Juma Ali Khatib wa chama cha ADA-TADEA aliyepata kura 392 sawa na asilimia 0.08,na Hamad Rashid Mohamed wa ADC aliyepata kura 996 sawa na asilimia 0.20,”alisema
Amesema mgombea mwingine wa urais wa Zanzibar Mussa Haji Kombo wa chama DP aliyepata kura 106 sawa na asilimia 0.02 na Hamad Mohammed Ibrahim wa UPDP aliyepata kura 181 sawa na asilimia 0.04.
Mgombea mwingine ni Mohammed Omar Shaame wa UMD aliyepata kura 104 sawa na asilimia 0.02 na Hussein Juma Salum wa TLP aliyepata kura 142 sawa na asilimia 0.03 na Issa Mohammed Zonga wa chama SAU aliyepata kura 102 sawa na asilimia 0.02.
“Mfaume Khamis Hassan wa chama cha NLD amepata kura 122 sawa na asilimia 0.02 huku Khamis Faki Mgau wa N.R.A alipata kura 160 sawa na asilimia 0.03 na Ameir Hassan Ameir wa Demokrasia Makini alipata kura 133 sawa na asilimia 0.03 pamoja na Shafi Hassan Ameir wa chama cha DP alipata kura 106 sawana asilimia 0.02,”alisema
Amesema Said Issa Mohammed wa CHADEMA alipata kura 1,702 sawa na asilimia 0.34 pamoja na Othaman Rashid Khamis wa chama cha CCK aliyepata kura 2,235 sawa na asilimia 0.45
More Stories
Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Ubelgiji lafanyika Dar
CCM kuhitimisha kampeni kwa kishindo
Walimu elimu ya lazima watatakiwa kuwa wabobezi kwenye masomo wanayofundisha