January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwili wa mtoto wa Diwani kuzikwa leo

Na Mary Margwe, Simanjiro

Mwili wa mtoto Kennedy Marco Munga (19) aliyefariki kutokana na ajili ya gari Aprili 18, Mwaka huu unatarajiwa kuzikwa nyumbani kwao katika Kitongoji cha Cha Orkiloriti Kijiji Cha Namaruru Kata ya Naberera Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

Marehemu Kennedy Marco Munga ni mtoto wa Diwani wa Kata ya Naberera Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara Marco Munga.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa, Diwani Munga alisema mwili wa marehemu mtoto wake Kenned umefuatwa katika hospitali ya KCMC, alikokua akipatiwa matibabu.

Awali Diwani Munga amesema Marehemu Kennedy ni mtoto wa kwanza kati ya watoto watano, na alikua akisoma chuo cha Famasia kiitwacho Paradigms College Of Science kilichopo Jijini Dar Es Salaam ambapo alikua Mwaka wa pili.

” Mtoto wangu alipata ajali ya gari Aprili 5, Mwaka huu tukampeleka hospitali ya Wilaya Orkesment baadae usiku tukampeleka KCMC ndipo ikagundulika amevunjika pingili za shingo mbili namba tano na namba sita, akafanyiwa upasuaji Aprili 7 na akawekewa chuma na akaonyesha kupona dalili nzuri ya kupona, ndipo baadaye hali ya mtoto ikabadilika ghafla na kufariki April 18, Mwaka huu ” amesema Diwani Munga.

” Hakika sina namna nitasema nini mimi, Kennedy si muda mrefu nilitoka kuongea naye na kwenda kupata ajali, mwanangu ameniachia pengo kubwa lisiloweza kuzibika milele, hakika namuachia Mungu mwenyewe, nitasema Nini sasa? amehoji Diwani Munga.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Baraka Kanunga amesema wako pamoja na familia ya Marehemu katika kuomboleza msiba na mtoto Kenned, aliyeiachia majonzi makubwa familia hiyo.

“Marehemu ninamfahamu na mwanangu pia, hakika ametuumiza sana sana, kifo chake kila mmoja amebaki tu ameduwaa, maana ni kama alitupa moyo baada ya kufanyiwa upasuaji, lakini jali ndipo ilipobadilika na kuaga Dunia” amesema Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo.

Hata hivyo Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Joseph Lyimo amesema amesikitishwa sana baada ya kupokea taarifa ya kifo Cha mtoto wa Diwani wa Kata ya Naberera Marco Munga.

Lyimo amesema Diwani Munga ni Rafiki yake wa karibu, hivyo Marehemu Kennedy kwake ni kama mtoto wake, hivyo amesema Yuko pamoja na familia katika kuomboleza kifo cha mtoto Kennedy.