Na Heri Shaaban , TimesMajira Online
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi CCM kata ya CHANIKA William Mwila amesema mikakati ya Chama cha Mapinduzi Chanika Mapendekezo yao kuigawa kata tatu kutoka kata moja kwa dhumuni la kusogoza huduma kwa wananchi.
Mwenyekiti William Mwila alitoa mapendekezo hayo katika kikao cha Halmashauri Kuu ya kata ya Chanika walipokuwa wakijadili mambo mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ya chama.
“Tunaelekea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024 kutokana na ukubwa wa kata yetu yenye mitaa minane mapendekezo yetu kuongeza mitaa kutoka minane mpaka kufikia mitaa 16 na kuongeza kata tatu kutoka kata moja iliopo sasa katika kikao cha Maendeleo ya Kata WDC tumeshapitisha .Mapendekezo haya ” alisema Mwila.
Mwenyekiti Mwila alisema Chanika ina wakazi zaidi ya Elfu 75,000 wananchi ni wengi na kata kubwa hivyo tunaigawa kwa ajili ya kusogeza huduma bora kwa wananchi waweze kupata huduma za kijamii karibu na makazi yao.
Akizungumzia uchaguzi wa Serikali za mitaa alisema Mikakati yao walivyojipanga ccm itashika dola mitaa yote minane na mitaa mipya ikiongezwa ikawa mitaa 16 Chama cha Mapinduzi kinaendelea kushika dola wamejipanga vizuri na kudumisha umoja na mshikamano
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilala Said Sidde alitoa Baraka zake Kata ya Chanika kugawanywa kwani sawa na Jimbo ina idadi kubwa ya wakazi hivyo alipongeza Kamati ya Maendeleo ya Kata WDC kwa kutoa baraka za kuigawanya Kata hiyo .
Akizungumzia uhai wa Chama cha Mapinduzi aliwataka waongeze wanachama wapya na kuwasajili katika mfumo wa kadi za kisasa za electonic zikiwemo za Jumuiya zote ,Wazazi, Vijana na UWT.
Alisema uchaguzi wa chama umeisha hivyo aliwataka Chanika kujenga umoja na kuakikisha chama cha Mapinduzi CCM kinashika dola katika chaguzi zake zote ikiwemo Uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa Rais wabunge na madiwani mwaka 2025.
Katibu wa CCM Chanika Yahaya Matumbo alimpongeza Rais DKt .Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa kata ya Chanika katika miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya na sekta ya Elimu bila kusahau miundombinu ya Barabara kwa sasa chanika wanajivunia Serikali ya awamu ya sita kwa kutatua kero za wananchi.
Alitumia fursa hiyo kumpongeza Mwenyekiti wa ccm kata ya Chanika William Mwila kwa kukijenga chama vizuri ambapo ametekeleza ahadi zake zote ndani ya chama kwa kujenga ofisi za chama pamoja vyoo sehemu zenye changamoto zote amezitatua na Chanika ipo Salama.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â