Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Dodoma
MWENYEKITI wa mtaa wa Chinyoyo kata ya kilimani,Jijini Dodoma,Faustina Bendera amepiga marufuku wananchi wa Mtaa wake kuacha mara moja kuchota mchanga katika miundombinu ya barabara zote za mtaa wa Chinyoyo kwakuwa ni uharibifu mkubwa wa barabara za mtaa.
Bendera ametoa Kauli hiyo jijini hapa leo, Disemba 11,2024 baada ya kuona baadhi ya wananchi wakichota mchanga baada ya mvua kunyesha hivi karibuni.
“Hivi karibuni baada ya mvua kunyesha kuna wananchi wameanza tabia ya kukusanya malundo ya mchanga katika barabara za mtaa Sasa ninawaambia ni marufuku kumwona mwananchi yoyote akisomba mchanga katika barabara za mtaa na yoyote tutakaye tutakayemkuta anachota mchanga tutamkamata na kumchukulia hatua kali za kisheria ikiwa kupigwa fani na kupelekwa mahakamani”amesema.
Aidha Mwenyekiti huyo amesema wanaotaka kusomba mchanga waende kwenye mtaro mkubwa unaujulikana kama mtaro wa wizara ya afya kwakuwa kuna mchanga unaoletwa na maji ya mvua pia watakuwa wamesaidia kuusafisha mtaro huo.
Mbalimbali na hilo mwenyekiti huyo amewataadharisha wananchi katika kipindi hiki cha mvua kuhakikisha wanafanya usafi katika maeneo yao ya nyumbani na mtaani ili kuhakikisha wanaepukana na magonjwa ya kuharisha (kipindupindu) ambacho kwa tarifa zilizopita tayari kimeshabisha hodi jijini Dodoma na kusababisha vifo.
Aidha Bendera amewasisitiza wananchi kuhakikisha wanatunza miundombinu ya barabara zote za mtaa na kuwa wanatoa taarifa za maafa yoyote yanatokana na mvua hizo zinazoendelea kunyesha hapa Jiji Dodoma.
More Stories
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa
Mgeja aipongeza CCM kwa uteuzi Wagombea Urais