January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diwani aliyemaliza muda wake Francis Mtega amefanikiwa kutetea kiti chake na kupata ushindi wa kishindo

Mwenyekiti wa Halmashauri apita kwa kishindo kura za maoni CCM

Na Esther Macha, TimesMajira Online, Mbeya

ALIYEKUWA Diwani Kata ya Chimala na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Francis Mtega amepita kwenye kura za maoni kwa kishindo .

Mtega ameibuka mshindi kwa kupata Kura 166 huku mgombea wa pili akiwa ni Charles Komba aliyepata kura 22, Peter Nselu 08 pamoja na Ibrahim Ngailo aliyeambulia kura 05.

Katika mchakato huo wa kura za maoni kulikuwa watia nia 04 na wapiga kura 201 .