May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenyekiti wa CCM Ilala awasihi wahitimu

Na Bakari Lulela, TimesMajira Online

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) kata ya Ilala Mkoani Dar es Salaam Ubaya Chuma amewasihi wahitimu wa chuo Cha Amana Vijana center kutumia taaluma zao vizuri ili ziwaletee mafanikio ndani ya jamii.

Akizungumza katika mahafali ya 17 Mkoani humo Ubaya Chuma ambaye alikuwa mgeni rasmi akimuwakilisha MWENYEKITI wa CCM Mkoa Kate Kamba amesema chuo hicho kimekuwa chuo pekee kinachowatimizia Vijana kufikia matarajio yao.

Jumla ya wahitimu katika chuo hicho walikiwa 248 Kati ya hao wasichana ni 196 huku wavulana wakiwa 42 ambapo walipatiwa vyeti pamoja na mbinu mbalimbali zitakazo wasaidia kupata ajira ikiwemo nidhamu,utiifu na umoja.

“Tunategemea mafunzo haya mliyoyapata Mahali hapa yatakuwa nguzo bora katika maisha yenu huko muendako hivyo inatosha kusema nyinyi mshakuwa mabalozi Wazuri wa kuweza kukiletea sifa chuo Cha amana Vijana center,” amesema Chuma

Aidha Ubaya Chuma amesema kupitia ujuzi mlioupata amewapongeza walimu kwa juhudi zao za kuwawezesha Vijana kupata ujuzi na maarifa yanayoweza kuwa na tija ndani ya jamii na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa chuo hicho Philipo Ndokeji amewataka wahitimu kuzingatia nidhamu na maarifa waliyoyapata kuwa ni nguzo huko wanakokwenda kwa kuwa ujuzi wamekwisha upata.

Mkuuu huyo amewataka Vijana wengine wanaopenda kujiunga na mafunzo hayo, amesema mafunzo hayo yanatolewa bure ambapo Kuna kozi ya hoteli managementi, kiingereza, mapambo, ufundi Bomba, ufundi umeme wa majumbani, komyuta,cherehani na udereva.

Nae Mkuu wa chuo Selestine Enock amewahimiza wahitimu hao wazingatie mafunzo ili waweze kujiaji wenyewe ambapo amesema kuwa karne hii ni ya uchumi wa viwanda hivyo wajiegemeze katika kutengeneza viwanda vidogo vidogo kwa maendeleo yao na vizazi vyao.