January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenyekiti UWT atunukiwa Shahada ya Uzamivu

Na Heri Shaaban

MWENYEKITI wa Umoja wanawake UWT Mkoa Njombe ,Scholastika Kevela, ametunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika masuala ya fedha Chuo Kikuu Huria.

Mwenyekiti wa UWT Scholastika Kevela, alisema ameweza kusoma PhD kwa utu uzima sio kazi nyepesi kupata PhD ambapo aliwataka wanawake wa Tanzania kuinuka kusonga mbele .

“Nampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fursa ya mikopo ya Elimu ya juu kuwezesha Watanzania kujiendeleza katika sekta ya Elimu  naomba wale wasiofikia kiwango hicho waweze kusoma”alisema Kevela.

Kevela alisema yeye ni Mwanamke Mwanasiasa ameweza kusoma shahada ya Uzamivu Phd katika masuala ya fedha kwa ajili ya wanawake wa Mkoa Njombe aweze kuwasaidia kiuchumi waweze kujikwamua kichumi.

Alitoa ushauri kwa Serikali waongeze mitaji kwa Taasisi za Mikopo vijijini waweze kuwainua wanawake kiuchumi waweze kukopa kwa wingi wakuze mitaji yao ya biashara .

Katika hatua nyingine alitoa pongezi kwa viongozi wa Umoja wanawake UWT Taifa, Mery Chatanda na Zainabu Shomary kwa kuwaongoza vizuri Wanawake wa UWT kuweza kufikia malengo yake.

Wakati huohuo alimpongeza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa ushindi wa Kishindo katika uchaguzi wa Serikali za mitaa nchini ambapo ccm imeibuka kidedea katika chaguzi hizo.