June 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenyekiti UWT Mkoani Arusha atoa msaada kwa familia zaidi ya elfu moja

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake (UWT) kata ya Kisongo Mkoani Arusha, Vaileth Ngowo amefanikiwa kutoa msaada wa unga kwa wanawake pamoja na wahitaji kwa familia zaidi ya elfu moja huku lengo likiwa ni kudumisha upendo na amani.

Akikabidhi misaada hiyo ambayo ni kilo tatu tatu za unga mapema jana Vaileth alisema kuwa lengo halisi ni kuweza kunusuru familia hizo kupata Mlo japo kidogo kutokana na baa la njaa ambao limeshamiri kwa Sasa Vaileth alisema kuwa safari ya kuisaidia jamii ni safari ambayo Kila mmmoja anatakiwa aangalie kuwa anapita kwa njia ipi kwa kuwa jamiii nyingi bado zinakabiliwa na changamoto.

Alisema kuwa hata kwa waliofanikiwa wanatakiwa wahakikishe kuwa wanakuwa sehemu ya jamii kwa kuweza kuwapa maitaji japo kidogo na endapo kama watafanya hivyo wataweza kunusuru jamii dhidi ya majanga kama vile njaaa.

“Leo nimewiwa kufanya Jambo hili ambalo ni msaada kwa familia hizi kama wote tunavyojua ni kuwa wapo baadhi ya familia halizao ni duni Sana na ni kutokana na ukosefu wa mvua ambazo hazijanyesha,nimetoa kama sehemu ya faida kutoka kwenye moja ya kazi zangu hapa Kisongo ili kuonesha ummma tunaweza kuisaidia sisi kwa Sisi na Nina shauri kuwa ni vyema sasa jamiii iige huu utaratibu”aliongeza.

Wakati huo huo alimshukuru Raisi Samia Hassan kuweza kushusha bei ya maindi kwa baadhi ya maeneo hali ambayo nayo imeleta Uraisi kwa baadhi ya familia hususani katika kata hiyo ya Kisongo.

Alihitimisha kwa kusema kuwa bado ana mikakati mbalimbali ya kuweza kuisaidia kata hiyo ya Kisongo ikiwa ni pamoja na kuleta Suluhu dhidi ya changamoto mbalimbali ambazo zipo.

Akiongea kwa niaba ya wananchi ambao wamepewa msaada huo, Nipaely Samweli alimshukuru sana mwenyeki huyo kwa kuweza kuwakumbuka waitaji wa kata hiyo kwa kuwapa Unga ambao wanaweza kutumia kwa familia zao Nipaely alisema kuwa waliopokea msaada huo ni walengwa kabisa kwa kuwa wengi wao ni wazee ambao kwa kweli hawana nguvu za kutembea na kwenda kujitafutia na wengi wao walikuwa wanatumia na kutegemea kilimo Ila mvua zilikosekana.

“Kwa niaba ya kina mama hapa nasema asante Sana na sasa tufungue fursa kwa kina mama wengine ambao Wana uwezo kidogo waweze kwenda kwa jamii ambazo ni wahusika wa mabaa kama vile njaa na changamoto nyingine tusisubiri Serikali pekee”aliongeza