Na Mary Margwe, TimesMajira Online, Naisinyai
MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Kiria Ormemei Laizer ameunga Mkono juhudi za Bilionea Laizer kwa kuchangia mifuko100 kati ya 200 aliyoahidi kwa ajili ya kujengea bweni la shule ya Awali na Msingi ya Saniniu Laizer.
Mwenyekiti Kiria amekabidhi mifuko ya saruji jana kwa mbele ya uongozi wa Kijiji ,Kitongoji na kumkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Swedefrida Msoma, iliopo kitongoji cha Namelock kijiji cha Naepo kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Alisema aliahidi kutoa mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa bweni wa Shule ya awali na Msingi ya Saniniu Laizer( English Medium) ,na hivyo kukabidhi mifuko 100 ya saruji, huku mifuko mingine 100 atakabidhi mwishoni mwa wiki.
” Niliahidi kutoa mifuko 200 ya saruji kwaajili ya ujenzi wa bweni wa Shule ya awali na Msingi ya Saniniu Laizer (English Medium) na leo hii nimetekeleza kutoa mifuko 100 kati ya 200 ya saruji, mingine 100 nitaikamilisha mwishoni mwa wiki hii ” amesema Kiria.
Aidha amesema mifukon100 ya saruji aliyoanza kutoa itasaidia kuanza Utekelezaji wa ujenzi huo wa bweni la shule hiyo kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wanaotoka umbali mrefu kuifikia shule ili waweze kulala shuleni hapo na kupata Elimu kikamilifu.
” Na hii ni jitihada ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wawekezaji hususani Bilionea Laizer,nkwambakwamba tuko pamoja na Chama Cha Mapinduzi,nimejitoa Kwa nguvu zangu zote kuhakikisha naunga mkono jitihada za Bilionea Laizer na wananchi Kwa ujumla” ameongeza Kiria.
Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya Awali na Msingi Saniniu Laizer, Swedefrida Msoma, amemponge na kumshukuru Mwenyekiti Kiria kwa moyo wake wa kujitolea mifuko 100 kati ya 200 aya saruji alioahidi kutoa kwao.
Msoma alisema Kiria amekua ni mtu mwenye Moyo wake, kwani sio mara yake ya kwanza kunitoa kuisaidia shule hiyo, kwani tayari alishajitolea kujenga hiko la shule na vitu vingine vingi.
“ Hatuna Cha kusema dhidi ya kumshukuru na kumpongeza Mwenyekiti wetu wa CCM Wilaya ya Simanjiro Mh.Kiria kwa kujitolea mifuko hiyo ya saruji 100 ambayo itakua imefunguka Milango ya wadau wengine nao kuweza kujitokeza kuisaidia shule hiyo.
Aidha mchango wa Kiria utakuwa ni mwanzo mzuri wa kuanza Utekelezaji wa ujenzi wa bweni la wanafunzi wa shule hii, wakati wakiemdelea kusubiri mifuko mingine 100 mwishoni mwa wiki hii” amesema Msoma.
Akiongea kwa niaba ya wananchi Diwani wa Kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara Mh. Taiko kurian Laizer amemshukuru Kiria Ormemei Laizer kwa jitihada zake lakini kubwa la kuendelea kujitoa katika michango mbalimbali kwa jamii.
” Tunamshukuru Mwenyekiti Kiria kwa kuonyesha uzalendo Kwa jamii ndani ya nje ya Wilaya hii, amekua akijitoa kusaidia katika mambo makubwa, muhimu Kwa jamii zetu, alipotoa Mwenyezi Mungu aendelee kumsimamia na kumuongezea maradufu” amesema Diwani Taiko.
Naye Mwenyekiti wa Kitongoji Cha Namelock Ikayo Kurian alisema sasa wakati umefika wa jamii mbalimbali nazo kuweza kuona mfano wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Kiria.
Aidha amesema kutoa ni Moyo na sio utajiri, hivyo hata mtu akitoa mfuko mmoja wa saruji Bado utasaidia kufanya jambo katika ujenzi, si mpaka ipatikane mifuko kama aliyotoa Mwenyekiti Kiria.
Hata hivyo ikumbukwe kuwa Shule ya Awali na Msingi ya Saniniu Laizer ya mchepuko wa Kingereza ipo Kitongoji cha Namelock Kijiji cha Naepo Kata ya Naisinyai, na imejengwa na Mfanyabiashara maarufu wa Madini ya Tanzanite Mji Mdogo wa Mirerani Bilionea Saniniu Laizer kwa gharama ya sh.Mil. 466.8 na kisha kuikabidhi Serikali namomJanuari 2021.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa