Na Penina Malundo,Timesmajira. Online
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala, Mohamed Msophe ameanza rasmi ziara yake ya siku tano katika wilaya hiyo kwa lengo la kuangalia utendaji wa kazi wa viongozi na kutoa shukrani zake za kuchaguliwa kuongoza wilaya hiyo.
Pia amesema mpango alionao kama Jumuiya ni kuongeza idadi ya wanachama katika Jumuiya yao na kuhakikisha wanatoa mafunzo mbalimbali, ikiwemo masuala ya uongozi na ujasiriamali kwa viongozi wote wa Jumuiya Wazazi Wilaya ya Ilala.
Msophe amesema ni vyema viongozi wakipata mafunzo hayo, ili kuweza kuongezea uelewa katika majukumu yao ya kazi.
Amesema anatarajia ziara yake kuanzia katika Jimbo la Ukonga kwa kukutana na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala wanaotokea katika Kata za Msongola, Zingiziwa, Chanika, Buyuni, Pugu, Pugu Station pamoja na Majohe.
“Nitoe shukrani zangu za dhati kwa wajumbe wote wa Mkutano Mkuu kwa kunichagua kuwa Mwenyekiti, nawashukuru nimekuja kuwashukuru na kusikiliza kero zenu, ziara yangu hii itakuwa ya siku tano kutembea wilaya nzima kuwashukuru wajumbe wote na kutoa dira ya Jumuiya yetu,” amesema.
Msophe amesema katika kuendeleza ujenzi wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Ilala, amenunua jumla ya kadi 1,800 na kumkabidhi Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala kwa ajili kuzigawa katika kata zote 36 za Wilaya ya Ilala.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa