Na Mwandishi wetu
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Balozi Mstaafu Ali Idi Siwa, ametembelea banda namba 13 la ushirikiano baina ya NSSF na PSSSF kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mfuko katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ‘Sabasaba’ yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere. Balozi Siwa alipata maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na NSSF na PSSSF.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Balozi Mstaafu Ali Idi Siwa, amempongeza na kumkabidhi Joyce Sungura, kadi ya uanachama wa NSSF baada ya kujiunga wakati alipotembelea banda la NSSF katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ‘Sabasaba’ yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. NSSF inashiriki katika maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi wakiwemo wakulima, wavuvu, wafugaji, wachimba wadogo wa madini, mama lishe, bodaboda na wajasiriamali wengine wote ambao wanapofika katika banda hilo wanapewa elimu na kuandikishwa kuwa wanachama wachangiaji.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Balozi Mstaafu Ali Idi Siwa, amekutana na Kamishna wa Polisi, Utawala Menejimenti ya Rasilimali Watu, CP Suzan Kaganda pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Wakala Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar, Juma Burhan Mohamed, alipotembelea Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ‘Sabasaba’ yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, nakujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mfuko katika maonesho hayo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Fatma Hamad Rajabu, ametembelea banda namba 13 la ushirikiano baina ya NSSF na PSSSF kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ‘Sabasaba’ yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
Matukio katika picha
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba