Na Heri Shaaban,Timesmajiraonline,Temeke
MWENGE wa Uhuru umezindua Miradi saba ya maendeleo Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es salaam yenye thamani ya shilingi bilioni 17.
Akizungumza jijini hapa leo Juni Mosi,2025 mara baada kuzinduliwa kwa miradi hiyo ya maendeleo Mkuu wa wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda ametaja katika miradi hiyo iliyozinduliwa na kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa,Ismail Ally Ussi kuwa ni Mradi wa ujenzi wa barabara Masaki,Kituo cha Polisi Tuangoma na mradi wa shule ya sekondari Magaya.
Aidha Mapunda ametaja miradi mingine kuwa ni Kituo cha Vijana Mabegi House,Mradi wa Hospitali ya Wilaya,Shule ya Sekondari Yombo Vituka na Uzinduzi wa Mradi wa Wapinga Rushwa ikiwemo taarifa ya Lishe kukagua shughuli za lishe.
“Manispaa yetu leo imezindua miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 17 fedha za maendeleo za mapato ya ndani tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuleta pesa nyingi za miradi ya maendeleo Manispaa yetu “amesema Mapunda.
Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Mbagala Abdalah Chaurembo amesema wanamshukuru Rais kwa kutoa pesa nyingi za miradi ya maendeleo wamejenga kituo cha Polisi cha Tuangoma kituo daraja C lakini kitapewa daraja D kitakuwa kinajitegemea .
Mbunge Chaurembo amesema Rais amefanya makubwa mwezi Oktoba yeye na wananchi wake watamlipa kwa kupiga kura nyingi.
“Jimbo la Mbagala limezaa jimbo jipya la Chamazi Mkoa Dar es Salaam kwa sasa maendeleo yote Serikali wataelekeza jimbo jipya la chamazi nawaomba wananchi muwe na imani ya ilani ya chama cha Mapinduzi CCM,”amesema Chaurembo.
Naye Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ussi,amepongeza Manispaa ya Temeke kwa kufanya kazi nzuri katika kusimamia miradi ya maendeleo kwa fedha za ndani ambapo amesema mwenge wa uhuru umeleta heshima kubwa Tuangoma kwani imekuwa kiuchumi hivyo Manispaa imelazimika kujijenga.
Mwenge wa Uhuru umetokea Mkoa wa Lindi umewasili mkoa Dar es Salaam kuzindua miradi ya maendeleo kuanzia Juni Mosi mpaka Juni 5,2025 kabla kukabidhiwa Mkoa Tanga,ambapo ulipokelewa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Lindi Zainab Terack.
Awali Chalamila alisema mwenge wa uhuru utazindua miradi 37 ya mkoa huo na kauli ikienda na kaulimbiu ya “Jitokeze Kushiriki uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa Amani na utulivu”. Â



More Stories
CCM kusimamia kitabu cha Hayati Songambele kiingie mtaani
Mwendokasi kuendeshwa na ENG kwa miaka 12
Vitongoji 284 Arumeru Mashariki vyafikiwa na umeme