June 5, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwendokasi kuendeshwa na ENG kwa miaka 12

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online

WAKALA wa Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (DART), umeingia mkataba wa miaka 12 na kampuni binafsi ya usafirishaji ya Emirates National Group (ENG) ya nchini Abu Dhabi kuendelea kuendesha mfumo wa BRT Jijini Dar es Salaam.

Mkataba huo ulisainiwa rasmi mwisho mwa wiki Mei 29, 2025 ukiashiria hatua muhimu katika jitihada za Serikali katika kuboresha huduma A usafirishaji wa Umma Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa DART Dkt. Athuman Kihamia, amesema ENG itachukua uendeshaji wa awamu ya kwanza ya mradi wa BRT na kuleta mabasi mapya 177 yatakayo rahisisha upatikanaji wa huduma za usafiri Jiji humo.

Imeelezwa kuwa, mchakato huo ulianza 2017 kupitia mfumo wa ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ( PPP), huku ikielezwa kuwepo kwa changamoto za kimajadiliano kuhusu kiwango cha nauli na mifumo mwingine ya kisuluhishi.

Mwaka 2020 Serikali ilitangaza upya sabuni ambapo kampuni 40 zilionekana kuwaislisha maombi na ENG kuibuka mshindi,ambapo hivi sasa tayari mchakato imekamilika na kampuni hiyo kuanza kazi hivi karibuni.