Na Patrick Mabula , Kahama.
MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza wa Sekondari ya Kata ya Nyihogo Wilaya ya Kahama, Freck Malulu (15 ) amefariki dunia baada ya kuangukiwa na mti wa Mwembe pamoja na kufunikwa na kifusi alipokuwa akichimba mchanga ili kwenda kuuza.
Mtendaji wa Kata ya Mhungula, Reuben Jonas amesema, mwanafunzi huyo alifariki juzi saa moja na nusu alipokuwa akichimba mchanga wa kuuza kwa kutumia mkokoteni wa kukokotwa na ng’ombe na wakati anachimba katika shimo lililokuwa chini ya mwembe, ghafla udogo ulititia na kisha mti huo kudondoka na kupondwa na kufariki papo hapo.
Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Mhungula, Elisha William amesema, baada ya kupewa taarifa ya tukio hilo na wasamalia wema, walikwenda eneo la tukio na kufanikiwa kunasua mwili wake ambao waliuzika baada ya uchunguzi wa Jeshi la Polisi.
Kufaatia kifo cha mawanafunzi huyo, Serikali ya mtaa wa Mhungula imepiga marufuku wananchi kuendelea kuchimba mchanga katika eneo hilo ambalo siyo rasmi na halijatengwa kwa kazi hiyo na yeyote atakayekaidi atachukuliwa hatua kali.
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam