Na Steven Augustino, TimesMajira Online, Tunduru
SERIKALI imemtaka mwekezaji wa kiwanda cha Kubangua korosho cha Korosho Africa LTD wilayani hapa, kuongeza ubanguaji wa zao hilo ili kuongeza ajira kwa wananchi na kwamba kama kimeshindwa kiseme, ili atafutwe mwekezaji mwingine.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme wakati akizungumza na wadau wa tasnia ya korosho kutoka katika mikoa hiyo, kwenye kikao cha wadau kilichofanyika Ukumbi wa Sky way mjini hapa.
Kwa sasa kiwanda hicho kinabangua tani 4,000 pekee kati ya tani 10,000, ambazo kiwanda kinaweza kuzibangua kwa mwaka na kuajiri zaidi zaidi wa wafanyakazi 2,000, badala ya wafanyakazi 600 waliopo kwa sasa.
Kwa mujibu wa Mndeme, jumla ya tani 24,525,814 zenye dhamani ya sh. bilioni 62.629 zilizozalishwa Mkoani hapa na kuuzwa kwenye msimu wa mwaka 2019/20 na kuvuka lengo kwa wastani wa kilo 1,525 sawa na asilimia 6.65 ya makadirio ya kukusanya kilo 18,000 katika msimu huo.
Mndeme amesema, jambo hilo linakwamisha kasi ya utendaji wa Serikali ya awamu ya tano, inayohimiza ujenzi wa viwanda nchini ili vitumike kusindika mazao yote ya wakulima na kuyaongezea thamani kabla ya kupelekwa sokoni.
Pia amewahimiza wakulima kuanzisha mashamba mapya ya mikorosho katika maeneo mbalimbali yaliyoko Mikoa ya Njombe, Mbeya na Ruvuma ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo kwenye misimu ijayo na kujipatia mapato makubwa ili kujikomboa kiuchumi.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro amesema sh. milioni 256.2 kati ya sh. milioni 288 zilizokuwa zimepotea na kudaiwa na wakulima wa Korosho wa wilayani hapa, zimerejeshwa na kulipwa kwa wakulima husika waliouza korosho zao kupitia mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani katika msimu wa mwaka 2019/20.
Amesema, fedha hizo zilizopotezwa na viongozi kutoka Vyama vya Ushirika vya Wakulima (AMCOS) 18, kati ya AMCOS 39 zinazohudumiwa na Chama Kikuu cha Wakulima Wilaya ya Tunduru (TAMCU).
Meneja wa Bodi ya Korosho Tawi la Tunduru, Shauri Mokiwa amezitaja changamoto ya ucheleweshaji wa vifungashio kwa baddhi ya AMCOS kabla ya msimu, hali iliyosababisha kuchelewa kwa kwa korosho kufika ghala kuu la mnada kwa wakati sahihi, ikiwa ni pamoja na kuchelewa kuanza kwa
minada ya korosho.
Changamoto nyingine ni wakulima kuhifadhi korosho katika vifungashio visivyo na ubora, ambavyo vimetumika kuhifadhia mazao mengine kama mahindi na kahawa.
More Stories
Wananchi Kiteto waishukuru Serikali,ujenzi wa miundombinu ya barabara
Watoto 61 wenye mahitaji maalum washikwa mkono
Mtoto wa mwaka mmoja na miezi kumi,adaiwa kubakwa na baba wa kambo