Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza
Wananchi jijini Mwanza wamehamasishwa kujiunga na huduma ya mfumo wa maji taka ili kutunza mazingira,kuepuka magonjwa ya mlipuko pamoja na kupunguza gharama za utapishaji wa vyoo.
Wito huo umetolewa na Ofisa Mawasiliano na Umma wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza(MWAUWASA)Hadija Mabula,wakati akizungumza na Timesmajira Online katika tamasha la Nishati Safi(Nishati Safi Festival), linalofanyika uwanja wa Nyamagana mkoani Mwanza.
Mabula amesema kuwa kuna faida nyingi ya kujiunga na mfumo wa maji taka ikiwemo kulinda mazingira,kuepusha mlipuko wa magonjwa mbalimbali yanayosavabishwa na uchafu pamoja na kupunguza gharama ya utapushaji wa choo pale kinapokuwa kimejaa kwani unaweza kutumia gharama kubwa kuita gari na mambo mengine.
Pia inaepusha athari mbalimbali mfano watoto wanaweza kudumbukia kwenye mashimo ya vyoo lakini katika mfumo huo si rahisi kwani mashimo hayatakuwepo.
“MWAUWASA tumeshiriki kwenye nishati safi festival kwa lengo la kutoa elimu na kuhamasisha watu kujiunga na mfumo wa maji taka ambao unapunguza gharama za utapishaji wa choo pindi kinapokuwa kimejaa kwani mfumo unatoa taka kutoka kwenye choo moja kwa moja kwenye chemba na kusafirishwa katika mfumo huo hivyo hakiwezi kukaa,”amesema Mabula.
Sanjari na hayo ametumia fursa hiyo kuwahimiza wale ambao wameisha jiunga na mfumo huo waache tabia ya kutupa taka ngumu katika vyoo vyao kwani vinasababisha kuharibu miundombinu ya mfumo huo.
“Mfano utupaji wa taulo za kike zilizotumika, vitambaa vinasababisha choo kuziba miundombinu ya mfumo huo inaweza kuvujisha maji yakatapakaa mtaani hivyo kusababisha mlipuko wa magonjwa hivyo watumie vizuri wasitupe taka hizo ngumu,”.
Aidha ameeleza kuwa ili kuunganishwa na mfumo wa maji taka lazima awe amejiunga na mfumo wa maji safi huku gharama za kujiunga na mfumo huo inategemea na umbali hivyo mtu atembelee ofisi za mamlaka hiyo ili kupewa mtu wa kumfanyia uchambuzi.
More Stories
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme