Judith Ferdinand,Timesmajira Online, Mwanza
Shule za msingi 11 pamoja na hospitali nne za Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza,zimekabidhiwa majengo ya vyoo na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza(MWAUWASA) huku lengo likiwa ni kuimarisha hali ya usafi wa mazingira katika taasisi hizo.
Mradi umetekelezwa kwa muda wa miezi 16 ukitarajiwa kunufaisha walimu na wanafunzi wapatao 14,062 katika shule za msingi Lake, Pamba, Nyakato, Kasota, Shigunga, Bugando, Bugarika, Buhongwa, Nyasubi, Nyabulogoya na Butimba huku hospitali zilizonufaika ni Buhongwa, Mbugani, Nyamagana na Bugarika.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Neli Msuya akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo kati ya MWAUWASA na Halmashauri ya Jiji la Mwanza kupitia Kaimu Mkurugenzi Peter Lehhet, yalioshuhudiwa na Mstahiki Meya wa Jiji hilo Sima Constantine aliyekuwa mgeni rasmi Machi 1, 2024.
Mradi huo umetekelezwa na MWAUWASA chini ya Mkandarasi kampuni ya M/s BENNET Contractors Ltd kwa ufadhili wa Serikali ya Tanzania pamoja na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) kwa gharama ya Tsh zaidi ya bilioni 2.
Msuya ameeleza kuwa mradi wa ujenzi wa vyoo katika shule za msingi, zahanati na maeneo ya wazi ulianza mwaka 2017 ambapo awali ulianza kwa majaribio kwa kujengwa vyoo katika shule za msingi 24 vyenye jumla ya matundu 336 katika halmashauri zote mbili za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.
“Awamu hii ya mwisho tumejenga vyoo katika shule za msingi 22 kati ya hivyo Wilaya ya Ilemela vyoo 11 na Nyamagana vyoo 11 vyenye jumla ya matundu 356,pia vyoo nane katika zahanati za Wilaya hizo ambapo kila moja imepata vyoo vinne,” ameeleza Msuya.
Hata hivyo amewasihi wanufaika wa mradi huo kuhakikisha wanautunza na kuulinda ili uendelee kutoa huduma inayokusudiwa.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi