Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA),Neli Msuya Mkurugenzi Neli ameeleza kuwa mtandao wa usambazaji maji katika eneo la Buhongwa wilayani Nyamagana mkoani hapa unaendelea kuboreshwa ili kuwezesha wananchi kunufaika na mradi wa Butimba.
Hayo ameyavainisha wakati ametembelea Kata ya Buhongwa kwa lengo la kukagua hali ya upatikanaji wa huduma za maji sambamba na kuzungumza na viongozi katika kata hiyo.
Neli amefanya ziara hiyo Mei 18, 2024 akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja, Salustia Kusekwa Meneja wa Kanda ya Nyegezi, Mhandisi Gombela Nswila na wasaidizi wake pamoja na timu ya ufundi na usambazaji wa maji.
Ambapo ameeleza kuwa hatua za muda mfupi, ni pamoja na mamlaka inalaza mabomba ya usambazaji maji kwa awamu katika mitaa mbalimbali hususani yenye changamoto ili kuboresha mfumo wa usambazaji.
“Katika hatua za awali za maboresho leo hii nimekabidhi kwa Mwenyekiti bomba kwa ajili ya kuboresha mtandao wa usambazaji wa maji kwa Mtaa wa Ng’washi,” amesema.
Akizungumza baada ya kupokea mabomba hayo Mwenyekiti wa Mtaa wa Ng’washi, Thobias Simon ameshukuru jitihada za MWAUWASA za kuhakikisha huduma katika mitaa hiyo inaimarika.
“Tunakushukuru Mkurugenzi kwa kututembelea na kutupatia bomba hizi zitakazoimarisha mtandao wetu wa maji, tunakupongeza kwa hili na kwa mipango uliyotueleza unayoendelea nayo. Tunakuahidi kuendelea kushirikiana nawe katika kufanikisha azma ya Serikali ya kumtua mwanamke ndoo ya maji kichwani,” amesema.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato