Na Steven Augustino, Tunduru
MWANAUME Athuman Maneti (43) amefariki baada ya kujinyonga hadi kufa katika tukio linalohusishwa na wivu wa mapenzi dhidi ya mke wake.
Mashuhuda wa tukio hilo wakiongozwa na diwani wa Kata ya Namiungo, Salima Limbalambala, waliliambia gazeti hili jana kwamba marehemu alichukua uamuzi huo usiku wa kuamkia Aprili 11, mwaka huu akiwa nyumbani kwake.
Habari zaidi zinaeleza kuwa kabla ya tukio hilo kulitokea ugomvi baina ya wanandoa hao huku mwanaume akimtuhumu kuwa na mahusianao na mwanaume mwingine.
Walisema baada ya tukio hilo walitoa taarifa kwa uongozi wa kijiji na baadaye Polisi ambao walifika na kufanya uchunguzi kisha kuruhusiwa kufanya mazishi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Saimon Maingwa alithibitisha kutokeo kwa tukio hilo na kwamba wanaendelea kufanya uchunguzi.
Aidha Kamanda Maigwa aliwataka wananchi kujipa nafasi ya kutuliza akili zao ikiwa ni pamoja na kuomba ushauri kwa wenzao namna ya kuhimili maudhi ya wenzi wao pindi inapotokea ugomvi kati yao.
More Stories
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam
MSF ilivyojidhatiti kusaidia serikali katika utoaji wa huduma za afya