January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwanasiasa mkongwe afariki Dunia

Na Bakari Lulela,Timesmajira

MWANASIASA  mkongwe wa Chama cha Mapindizi (CCM)ambaye ni mjumbe wa chama hicho shina namba 7   Sadiki Nassoro (81) amefariki dunia na kuacha pengo kubwa katika mtaa alipokuwa akiuongoza.

Marehemu huyo anatarajia kuzikwa Leo 10 januari 2025  katika makaburi yaliyoko maeneo ya Kipera huko mkoani  Morogoro.

Akizungumza jijini Dar es salaam , mahala ambapo marehemu alipokuwa akiishi Diwani wa kata ya Hananasifu  Willfred Nyamwija ambaye alimuwakilisha diwani wa kata ya Tandale amesema kuwa chama chetu (CCM) kimepoteza mtu mahiri katika medani za siasa.

“Marehemu alikuwa mwanaharakati wa siku nyingi katika masuala ya siasa hivyo tuyaenzi Yale mazuri aliyoyafanya katika kipindi chote cha uhai wake,” amesema Nyamwija 

Aidha Nyamwija amesema kuwa marehemu alikuwa mpenda maendeleo, msikivu na mpigania haki katika jamii aliyokuwa akiiongoza. kifo chake kilimkuta akiwa nyumbani akitokea hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa alipatiwa tiba dhidi ya maradhi mapafu kukaa maji.

Hivyo marehemu Mzee Sadiki Nassoro pamoja na harakati zake katika medani za siasa alikuwa muumini wa dini ya kiislamu ambapo ameacha mjane mmoja na watoto watano( 5) mola mpumzishe Mzee huyu mahala pema.

Kwa upande wake Jaffari Sadiki ambaye ni kijana wake amesema kuwa Baba yake alianza masuala ya kisiasa toka miaka ya themanini (80) na alikuwa mchapakazi kweli kweli.

 kabla ya kufikwa na mauti alipelekewa katika hospitali ya kigogo kwa matibabu lakini alipatiwa uhamisho na kuelekea katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es salaam na kupata unafuu ndipo umauti ulipomkuta.