May 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Johari ameungana na Viongozi mbalimbali nchini kushiriki kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Hayati Cleopa Msuya

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza S. Johari tarehe 11 Mei, 2025 ameungana na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Wananchi kushiriki kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati, Cleopa David Msuya katika Viwanja vya Karimjee, Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaongoza waombolezaji kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa Hayati Msuya.