MWANAMUZIKI Mkongwe kwenye muziki wa dansi hapa nchini, Hussein Jumbe amefariki dunia leo katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.
Jumbe aliyeitwa Mzee wa Dodo na Mtumishi aliwahi kupitia bendi za Tabora Jazz, Mara Jazz, Urafiki Jazz, DDC Mliman Park ‘Sikinde’ na TOT Band, Juwata Jazz na Mikumi Sound.
Jumbe alikuwa akisumbuliwa na kifua kwa muda mrefu. Mwanamuziki huyo mkongwe atakumbukwa kwa nyimbo nyingi alizozitunga baadhi zikiwa ni Nachechemea, Nani Kaiona Kesho, Isaya na Kiapo.
Msiba upo nyumbani kwa marehemu Twangoma Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio