November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwanamke mwenye ulemavu wa miguu aomba msaada wa kujengewa nyumba na choo

Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya

MWANAMKE mwenye ulemavu wa miguu mkazi wa Kata ya Tembela wilaya ya Mbeya ,Tabia Mwashilili ameiomba jamii na wadau kumsaidia mahitajimbali mbali ikiwemo kujengewa nyumba , choo ili aweze kuepukana namaisha duni ya kuishi kwa kuomba kwa muda mrefu kutokana na hali yaulemavu alionao.

Akizungumza na timesmajira leo nyumbani kwake Mwanamke huyo Mlemavu amesema hayo leo alipotembelewa na Taasisi ya Tulia trust kwa lengola kutoa msaada wa bati kwa mwanamke huyo .Mwanamke huyo amesema kuwa anashukuru sana kwa Dkt .

Tulia Acksonkumsaidia na kuomba wadau waendelee kumsaidia kwani maisha yake nimagumu hana nyumba wala choo na kusema yupo kwenye maisha hatarishisana .

“Naomba sana wadau ,jamii waendelee kunisaidia ili kuepukana na mamboya kuomba omba maana hata umri wangu umeenda sina nyumba sina choonipo kwenye mazingira hatarishi hata walipokuja walipokuja wageniwamenikuta nipo kuoga nyumba ya jirani hali yangi ndo hiyo nipokwenye mazingira magumu sana , huu msaada wa bati utanisaidia sanautakuwa msaada kwangu kwani sikutegemea kuzipata hizi bati “amesema Mwanamke huyo.

Akielezea zaidi Mwanamke huyo amesema kuwa alilima viazi akafanikiwakuuza na kujenga hiyo nyumba na kufikia hatua ya kuomba msaada wabati ili aweze kuezeka.

Diwani wa Kata Tembela Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya , JumaMwandangala amesema zawadi a ya bati iliyotolewa na Mbunge waMbeya mjini ni kubwa na kama alipangiwa adhabu kwa Mwenyezi Munguatampunguzia adhabu.Kwa upande wake Meneja wa Tulia Trust , Jackline Boaz amesema kuwawamefika kwa mama huyo kumwakilisha Spika wa Bunge la Jamhuri yaMuungano wa Tanzania,Dkt. Tulia Ackson kutoa msaada wa bati kwamwanamke huyo mlemavu kutokana na ombi lake la bati kwa Spika .

“Mwanamke huyu alianza kumtafuta Spika akiomba msaada wa Bati iliaweze kuezeka nyumba yake wakati akiomba msaada mwanamke huyo mlemavuhakuhitaji chochote zaidi ya Taasisi ya Tulia Trust kuona mazingiraanayoishi ili aweze kusaidiwa,fundi alipopiga hesabu ilionekana batisita ndizo zinatakiwa ili ziweze kukamilisha nyumba hii “amesema Meneja Tulia Trust.

Meneja Tulia Trust akisalimiana na Bi Tabia ambaye ni mlemavu nyumbani kwa mwanamke huyo kata ya Tembela.