November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Fedha kiasi cha Milioni mbili kilichookolewa kati ya Milioni 12.2 zilizo ungulia kwenye nyumba ya Martine Wandela mkazi wa Kitongoji cha Califonia Mji Mdogo wa Katoro Wilaya ya Geita(Picha na Mutta Robert)

Mwanamke aokolewa akitaka kujitosa kwenye moto kuokoa milioni 12

Na Mutta Robert, TimesMajira Online, Geita

SARAPIA Sarapia Charles mkazi wa Kitongoji cha Califonia katika Mjini Mdogo wa Katoro Wilaya ya Geita ameokolewa na wananchi akitaka kujitosa kwenye nyumba yake iliyokuwa inaungua kwani ya kutakia kuokoa sh.milioni 12.2 zilizokuwa zimehifadhiwa uvunguni mwa kitandani.

Akizungumza na TimesMajira,mwanamke huyo amesema nyumba hiyo imeungua Julai 23, mwaka huu, majira ya saa tatu asumbuhi akiwa kazini kwake dukani ambapo alipiwa simu na mme wake akimjulisha kupata taarifa za nyumba hiyo kuungua na kumuomba aende kunusuru fedha hizo.

Amesema mume wake alikuwa safarini hivyo yeye alilazimika kukimbia nyumbani na alipofika alikuta nyumba inaungua na akataka kuingia ndani ili anusuru fedha hizo lakini wananchi walimshika na kumzuia asiingie ili asipoteze maisha maana nyumba ilikuwa imeisha ungua sana.

Sarapia Charles amesema wamefanikiwa kuokoa kiasi cha milioni 2 tu kati ya 12 lakini na hata hizo zimeungua na kubaki vipande vipande na milioni 12 ziliteketea kabisa..

Martine Wandela ambaye ni mmiliki wa nyumba iliyoungua,amesema kuwa wakati ajali hiyo inatokea alikuwa amesafiri kuelekea Kata ya Bukoli Wilayani Geita na alipigiwa simu na mwananchi ambaye alimjulisha kuwa nyumba yake inaungua.

Amesema kuwa alimpigia mke wake na kumuomba awahi nyumbani kuokoa fedha hiyo iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya kununulia mpunga lakini mke wake alikuta nyumba imeungua kwa kiwango kikubwa na alipotaka kuingia ndani wananchi walimzuia.

Mmiliki huyo amesema kuwa wakati ajali hiyo inatokea msichana aliyekuwa nyumbani alisikia sauti kubwa kwenye switi ya umeme baada ya umeme kurudi ghafla kwa sababu ulikuwa umekatika,baada ya muda aliona moshi ndani ya vyumba ndipo alitoka nje na kuomba msaada kwa majirani.

Harrison Andrew Meneja wa tawi la Geita Benki ya CRDB amesema kuwa kuna hasara kubwa kiuchumi wananchi wanapo hifadhi fedha zao ndani ya nyumba zao bila kuzipeka benki kwa ajili ya kuhifadhiwa eneo salama.

Amesema kuwa kuhifadhi fedha nyumbani ni kuvuruga uchumi wa nchi kwa sababu fedha inaondolewa kwenye mzunguko wake na kusababisha madhara kiuchumi nchini .

Amewataka wananchi kuhifadhi fedha zao benki ili kuepuka hasara kazi hizo za kuungulia ndani ya nyumba zao lakini pia kuendeleza mzunguko wa fedha kiuchumi .

Amewataka wananchi wasiwe na wasiwasi ya kukosa huduma ya kupata fedha endapo wakitaka kuchukua fedha zao zinapokuwa benki kwa sababu sasa huduma zimesogezwa karibu kama mawakala wa mabenki wako mitaani muda wote na pia ATM zipo kila mahala na hata huduma kwa njia ya simu inapatikana.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Califonia Ernest Mwembeni amesema baada ya kupata taarifa za ajali hiyo alifika lakini nyumba ilikuwa imeungua sana huku akidai Jeshi la Zimamoto na Uokozi mkoa wa Geita lilifika lakini muda ulikuwa umeenda kwasababu na nyumba imeteketea sana.

Ameomba mamlaka husika kusogeza huduma ya Zimamoto katika mji huo kwani unakua kwa kasi na jeshi hilo kutoka Geita mjini ni mbali kuanza safari na kufika pale kwa umbali uliopo,unakuta madhara yameisha kuwa makubwa .

Zabrone Muhumha Kamishina Mwandamizi Msaidizi wa Jeshio la Zimamoto na Uokozi Mkoa wa Geita amewaomba wananchi kutumia benki kuhifadhi fedha zao ili kuepuka hasara pindi inapotokea ajali kama hizo kama hizo za Moto .

“Wananchi wasiweke vitu vya thamani kubwa nadani ya nyumba zao kama fedha wazipeleke benki na dhahabu waziuze kwenye masoko ya dhahabu ili kuepuka hasara kubwa kama ikitokea majanga kama haya ya moto” amesema Zabron.