January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Katibu wa CCM Wilaya Mpanda, Abdallah Kazwika akimkabidhi fomu za kugombea Ubunge jimbo la Mpanda Kati kwa tiketi ya CCM, Bathromeo Chilwa.

Mwanahabari Bathromeo Chilwa ajitosa Ubunge Mpanda Kati

Na Joyce Kasiki,timesmajira online

WANAHABARI wamechomoza katika siku ya kwanza ya uchukuaji fomu wakiomba kusimamishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba, mwaka huu.

Miongoni mwa wanahabari hao na kada wa CCM ni Bathromeo Chilwa. Zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu kwa upande wa CCM lilianza jana na linatarajiwa kuhitimishwa Julai 17, mwaka huu saa 10 jioni.

Chilwa ambaye kwa sasa ni Ofisa Habari wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) amechukua fomu leo akiomba kusimamishwa na CCM kuwania ubunge Jimbo la Mpanda Kati.

Chilwa alikabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa CCM Wilaya Mpanda, Abdallah Kazwika.