December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwanahabari ajitosa Ubunge Arusha Mjini, achukua fomu leo

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Arusha

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Arusha Mjini, Mwandishi Mwandamizi wa gazeti la Majira Pamela Mollel amechukua fomu ya kuwania kiti hicho.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu na Katibu wa Wilaya CCM Arusha, Denis Mwita katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Pamela amesema lengo kuu ni kushirikiana na wananchi wa Arusha kuleta maendeleo.

Pamela Mollel amesema atahakikisha anaisimamia ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika utekelezaji.