January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwanafunzi bora kidato cha nne aibuka shule ya Nguvu Mpya

Na Heri Shaaban , TimesMajira Online, Ilala

MWANAFUNZI Bora wa kidato Cha Nne 2022 Rahim Nasibu miaka (16) aibuka Mtaalam wa masomo matano yote anapata alama (A ) Mathematics ,civis ,Geograph ,Biology Phiysics katika shule ya kisasa ya Serikali Nguvu Mpya iliyopo Chanika Wilayani Ilala .

Akizungumza katika Mahafali ya 13 ya kidato cha nne shule ya Sekondari Nguvu Mpya Chanika Mwalimu wa Taaluma wa shule hiyo Oliva Osward amesema Mwanafunzi wake Rahim Nasibu alimpokea mwaka 2019 alikuwa na kipaji kizuri anajituma awali Wazazi wake walitaka kumwamisha lakini tukawapa moyo akawa anasoma mpaka amefika kidato cha nne .

“Nikiwa Mwalimu wa Taaluma katika shule hii ya Serikali nasimamia maendeleo ya Wanafunzi wote kitaaluma Mwanafunzi Rahim Nasibu ndio mwanafunzi wa kwanza Darasani anafanya vizuri masomo yote matano Mathematics ,civis ,Biology ,Geograph na Phiysics natamani huko mbele afanye vizuri zaidi katika masomo yake aweze kuwa kiongozi Bora katika Taifa letu ” amesema Mwalimu Oswald.

Mwalimu Oswald amewataka wazazi kushirikiana na Walimu na Wanafunzi Ili Wanafunzi waweze kusoma na kufikia malengo yao ikiwemo Serikali iweze kupata Wataalam mbalimbali wasomi waje kujenga Taifa .

MWANAFUNZI Rahimu Nasibu miaka 16 mwanafunzi Bora wa Shule ya Nguvu Mpya amesema kwanza anashukuru Mwenyezi Mungu ,Wazazi na Walimu kwa kumuwezesha kufanya vizuri kitaaluma Darasani matarajio yake kujiendeleza kielimu Ili aje kuwa Mtaalam wa Teknolojia .Mzazi wa Rahim Nasibu ,Joha Sultan, amesema mwanawe wamemlea katika maadili mema wanamtengea muda wa kusoma matarajio yao mtoto wake aweze kufika mbali zaidi .

Mkuu wa Shule ya Sekondari Nguvu Mpya Daniel Mwakyambiki, amesema Mwaka huu 2022 Wahitimu 376 wavulana 174 Wasichana 202 shule ya Nguvu Mpya Ina wanafunzi 2416 kati yake wavulana 1098 Wasichana 1318 idadi ya walimu waliopo 52 Wanaume 18 Wasichana 34Mwalimu Mwakyambiki amesema shule yake ya Sekondari Nguvu Mpya imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma kila Mwaka katika matokeo ya kidato Cha nne .

Amesema shule hiyo kitaaluma ipo vizuri Ina Walimu Wazuri wa masomo mbalimbali wanashirikiana na Walimu wake na Wazazi na Wanafunzi katika sekta ya Elimu wanasshirikiana na kuongeza ufaulu.

“Katika shule yangu nimekuwa nikishirikiana Walimu wangu na Wazazi Kila Mwaka ufaulu umeongezeka tunashirikiana pia na Afisa Elimu Halmashauri ya Jiji katika sekta ya Elimu na kutatua changamoto mbali mbali za shule ” amesema Mwakyambiki